Tuesday, September 11, 2012

Ligi Kuu ya Grand Malt Zanzibar: Bandari FC. yainyuka Malindi FC, 3-2.


Waamuzi na wachezaji wakiingia uwanja wa Amaan kuanza mchezo ambao Bandari waliibuka washindi wa mabao 3-2.

Wachezaji wa Timu za Bandari na Malindi wakiingia katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar jana kwa ajili ya  kuanza pambano.

Timu ya Bandari wakiomba dua.

Timu ya Malindi wakiomba dua.

Mshambuliaji Samir Khamis wa timu ya Malindi (No.8) akiwania mpira na mlinzi wa Bandari, Kassim hariri jana kwenye uwanja wa Amaan ambapo Bandari ilishinda mabao 3 - 2.

Mshambuliaji Amour Omar wa timu ya Bandari akiwa tayari kupiga shuti huku Samir Khamis wa Malindi (kulia) akiwa makini kumzuia. Hadi mwisho wa mchezo, Bandari 3 Malindi 2.

Mchezaji wa timu ya Malindi, Rajabu Rashid akipiga penalti na kuifungia timu yake bao la kwanza. Picha zote na Intellectuals Communications Limited

No comments:

Post a Comment