Saturday, September 15, 2012

NASHUKURU YA RECHO NAYO HIYOOOOO YAJA




Na Elizabeth John

MWANADADA anayetamba katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini, Rachael Haule ‘Recho’ ameachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Nashukuru’, huku akitaraji kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Recho alisema anamshukuru Mungu nyimbo zake zinapokelewa vizuri na mashabiki wake hivyo anajitahidi kukamilisha video ya wimbo huo mwishoni mwa mwezi huu ili kuwapa raha mashabiki wake.

“Muziki ni sehemu yangu ya kazi na sipendi mtu aizalau kazi yangu n asipendi kuwaudhi mashabiki wangu ili kuepukana na hili nimeamua niwe natoa nyimbo ambazo zimeenda shule ili nisiwachoshe wapenzi wangu,’ alisema Recho.

Recho alisema anawaomba mashabiki wake wasikae mbali na yeye kwani kuna vitu vingi ambavyo amewaandalia ambavyo anaamini zitakuwa ni burudani kwao.

Licha ya kutamba na kibao hicho, Recho alishawahi tamba na nyimbo zake kama, Upepo, Kizunguzungu n anyinginezo ambazo zinafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio

No comments:

Post a Comment