Saturday, September 15, 2012

NABISHA AIPELEKA RUNINGANI VIDEO YAKE YA NAJUA




Na Elizabeth John

MWANADADA anayetamba katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini, Beatrice Mathew ‘Nabisha’ (pichani) anajipanga kuachia video ya kazi yake inayokwenda kwa jina la ‘Najua’ ambayo inafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio kwa sasa.

Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam jana, Nabisha alisema katika wimbo huo amemshirikisha mkali wa muziki huo ambaye anamkubali sana kupitia kazi zake, Banana Zorro.

“Banana ni msanii ninayemkubali sana na nilikua na ndoto za kuimba naye tangu nikiwa mdogo namshukuru Mungu nimetimiza ndoto zangu, naamni kazi hii itafanya vizuri zaidi kutokana na uwepo wake,” alisema Nabisha.

Nabisha alisema, yupo katika michakato ya kuachia albamu yake ya kwanza itakayokuwa na nyimbo nane, ambayo bado hajaipatia jina kutokana ubora wa nyimbo ambazo zitapamba albamu hiyo.

Mbali na Najua, Nabisha alishawahi kutamba na nyimbo zake kama, Kidole gumba, Mapenzi ya kweli na nyinginezo ambazo zilimtangaza na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.

No comments:

Post a Comment