Saturday, September 15, 2012

VIDEO YA USHANIFAHAMU YA LINAH YAKAMILIKA




Na Elizabeth John

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Linnah Sanga anajipanga kuachia video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Ushanifahamu’ ambao unafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.

Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es salaam jana, Linnah alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa kazi hiyo ambayo anaamini itafanya vizuri zaidi kadri itakavyoendelea kusikika masikioni mwa mashabiki kutokana na ubunifu aliotumia.

“Nimeamua kufanya tofauti na kazi nyingine, hii itakuwa tofauti kidogo na naomba wapenzi wangu waendelee kunipa sapoti katika kazi zangu bado kuna vitu vingi ambavyo nimewaandalia,” alisema Linnah.

Alisema sehemu kubwa ya video ya kazi hii amefanya mjini Morogoro kwa lengo ya kubadilisha mazingira ili iwe na muonekano tofauti na kazi zake zilizotangulia.

Mbali na Ushanifahamu, Linnah anakumbukwa kwa nyimbo zake matata kama Lonely, Angalau, Fitina, Bora Nikimbie na nyinginezo ambazo zinafanya vizuri ka

No comments:

Post a Comment