Sunday, September 16, 2012

NTAIFICHA WAPI YA LINEX KUONEKANA VIDEONI


Na Elizabeth John
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Sunday Mangu ‘Linex’, anajipanga kuachia video ya wimbo wake unaokwenda kwa jina la ‘Ntaificha wapi’ ambayo inafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Linex alisema ndani ya wimbo huo kamshirikisha mkali wa muziki wa bongo fleva nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Pletinum’.

Linex alisema anaamini wimbo huo utafanya vizuri katika  soko la muziki na uwepo wa Diamond katika wimbo huo kutamsaidia yeye kuvuta mashabiki wengi kutokana na msanii huyo kupendwa na mashabiki wengi.

“Penye ukweli inatakiwa tuseme ukweli, Diamond ni msanii ambae anakubalika katika soko la muziki si ndani wala nje ya nchi hivyo anastahiri pongezi na ndio maana nimeamua kumshirikisha katika single yangu,” alisema Linex.

Licha ya kutamba na ngoma hiyo, Linex alishawahi tamba na nyimbo zake kama, Mama Halima, Moyo wa Subira, Mrembo, Aifola aifola na nyinginezo ambazo zinafanya vizuri katika tasnia ya muziki nchini.

No comments:

Post a Comment