Tuesday, September 11, 2012

SUPER D KUANDAA DVD YA KIDUNDA AKIWA KATIKA MASHINDANO YA OLIMPIC 2012



Na Mwandishi Wetu

KOCHA Kimataifa  wa mchezo wa ngumi wa Klabu ya Ashanti na Timu ya Mkoa wa Ilala Kimichezo, Rajabu Mhamila'Super D', anatarajia kuandaa CD ya bondia wa mchezo huo, Seleman Kidunda.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Super D alisema kuwa anatarajia kuandaa DVD hiyo ambayo itakuwa inaonesha matukio mbalimbali yaliyofanyika Mjini London wakati Kidunda alipokwenda kwenye mashindano ya Olimpic.

Alisema kuwa DVD hiyo inatarajiwa kuingia sokoni mwisho wa mwezi huu ambapo pia itaonesha kambi ya Kidunda wakati alipokuwa London.

Kocha huyo alisema kuwa anatarajia kuandaa DVD hiyo ili kuweza kutoa fursa kwa mashabiki na wapenzi wa mchezo wa ngumi, kuweza kuona matukio mbalimbali yaliyotokea na yaliyomhusisha Kidunda.

Alisema kuwa mashabiki pamoja na mabondia watajifunza mambo mengi kwa kupitia DVD  hiyo ikiwemo mafunzo ya mchezo huo pamoja na sheria zake ambazowadau wote wanapaswa kujua hizo taratibu na sheria za mchezo huo DVD ambayo itatoka mwishoni mwa mwezi huu.

"Ninatarajia kutoa DVD ambayo itakuwa inaonesha matukio mbalimbali yaliyotokea nchini London wakati Kidunda alipokwenda kwenye michuano ya Olimpic" alisema.

Kuanzia kambi aliyofikia mpaka alipokuwepo ulingoni akishiliki mashindano hayo hii ni historia ya pekee kwa tanzania ambapo iliwakilishwa na bondia mmoja ambaye ni selemani Kidunda katika DVD hiyo pia kutakuwa na mapambano mengine ya mabondia wa Tanzania waliowai kucheza nashindano ya kimataifa wakiwa nje ya Nchi

Pamoja na ndani ya nchi Super D ambaye utumia kufundisha mbinu mbalimbali za masumbwi kupitia DVD ambapo mpaka sasa amekwisha towa matoleo 16 kwa ajili ya mafunzo ya mchezo huo yakishilikisha mabondia  Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye, Nonito Donaire na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.


Super D usambaza DVD zake Katika Michezoya  ngumi  yote ambapo pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Mkoa wa Kimichezo wa Ilala, Rajabu Mhamila ‘Super D’ kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.Ndani yake wakiwemo mabondia wengi wanaotamba kitaifa na kimataifa

No comments:

Post a Comment