Tuesday, September 11, 2012

MASHINDANO YA NGUMI YA UBINGWA WA TAIFA KUFANYIKA SEPT 17-22/01212.


Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT)limeandaa mashindano ya ngumi ya ubingwa wa Taifa 2012 yatakayofanyika kuanzia jumatatu ya tarehe 17-22/09/2012 uwanja wa ndani wa taifa (indoor stadium) kila siku kuanzia saa 9.00 alasiri.

Awali mashindano hayo yalipangwa kuanzia Septemba 15, ila yalisogezwa mbele kutokana na uwanja wa ndani wa taifa kuwa na shughuri nyingine ya kimichezo ya ligi ya mpira wa kikapu.

Lengo la mashindano hayo ni kupata timu ya taifa ya ngumi yenye sura ya kitaifa ,itakayoshirikisha mikoa yote ya Tanzania bara, ili kuanza maandalizi ya mapema na ya uhakika kwa ajili ya kushiriki mashindano ya jumuiya ya madola 2014.

Aidha maandalizi hayo ni pamoja na kujiandaa kwa mashindano ya Afrika 2015, mashindano ya olimpiki 2016, ubingwa wa dunia na mashindano mbalimbali yatakayojitokeza kwa ajili ya kuwakilisha taifa.

''Hadi  leo jumla ya mikoa kumi na nane (18) imethibitisha kushiriki mashindano hayo, ambapo mikoa hiyo ni mikoa ya kimichezo ya Temeke, Kinondoni  na Ilala, mingine ni Ngome ya JWTZ,JKT, Magereza na Polisi. Mingine ni Pwani, Morogoro, Mbeya, Ruvuma, Dodoma, Kigoma, BukobaTanga, Arusha, Tabora na Mwanza''. alisemaa Makore

''Uongozi wa BFT licha ya kutopata udhamini wa uhakika wa kufanikisha mashindano hayo, kwa kushirikiana na wadau  balimbali tumejipanga vema kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa kiwango cha hali ya juu ili kufikia lengo la kupata timu bora ya taifa kwa wakati kwa maandalizi ya mapema, ambapo mashindano hayo yana takiwa kufanyika kwa bajeti ya milioni ishirini na sita (26,000,000/=)''. alisema. Makore

Mabadiliko ya ratiba ya mashindano itakuwa kama ifuatavyo:-
TAREHE
MUDA
TUKIO
16/09/2012

Timu zote kuwasili dare s salaam.
17/09/20123
1.00-4.00 Asb
4.00-5.00 Asb
5.00-7.00 Mch
Kupima uzito na afya,uwanja wa taifa wa ndani.
Zoezi la draw na bye na ratiba ya mashindano.
Semina kwa waamuzi,timu manaja,makocha kwa ajili ya kupatiwa kanuni na sheria za mashindano.
18/09/2012
1.00-2.00 Asb
8.00-2.00 Usk
Kupima uzito na afya,uwanja wa taifa wa ndani.
Gwaride la ufunguzi na kuanza mashindano hatua ya mtoano
19/09/2012
1.00-2.00 Asb
9.00-2.00 Usk
Kupima uzito na afya
Mashindano kuendelea hatua ya mtoano
20/09/2012
1.00-2.00 Asb
9.00-2.00 Usk
Kupima uzito na afya
Mashindano kuendelea kwa hatua ya robo fainali
21/09/2012
1.00-2.00 Asb
2.30-8.45Mch
9.00-2.00 Usk
Kupima uzito
Mkutano mkuu  wa BFT(indoor stadium)
Mashindano kuendelea hatua ya nusu fainali
22/09/2012
1.00-2.00 Asb
8.00-2.00 Usk
Kupima uzito na afya.
Gwaride la kufunga na kuendelea kwa mashindano hatua ya fainali.
23/09/2012

Timu zote kuondoka
Aidha ajenda za mkutano mkuu wa wanachama wa bft ni mbili tuambazo ni kupitia na kupitisha rasmu ya katiba ya BFT na maandalizi ya uchaguzi wa BFT wa kuwapata viongozi makiniwa kuongoza BFT kwa kipindi cha miaka mine kuanzia marchi 2013 kwa mujibu wa katiba .

Makore Mashaga
Katibu Mkuu BFT.,
   Mob:-0713/0784/0763/0773 -58 88 18
Email:- mashagam@yahoo.om

No comments:

Post a Comment