Tuesday, September 25, 2012

TFF: RUKSA KLABU KUCHEZESHA NYOTA WATANO WA KIGENI MECHI MOJA




 Kikosi cha kwanza cha Yanga kilichocheza na kushinda mabao 4-1 dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa. Kikosi hichi kinajumuisha wakali wote wa kigeni waliosajiliwa Yanga msimu huu; Yaw Berko (kulia waliosimama), Didier Kavumbagu (katikati nyuma), Mbuyu Twite (kulia waliochuchumaa), akifuatiwa na Hamis Kiiza na Haruna Niyonzima (wa pili kushoto waliochuchumaa).
DAR ES SALAAM, Tanzania

SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF), limesema ni ruksa kwa klabu yoyote kuwachezesha kwa pamoja wachezaji wote wakigeni waliosajiriwa na klabu katika Ligi Kuu ya Vodacom Tazania Bara.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa TFF Boniface Wambura alisema kuwa, sheria na kanuni za Ligi Kuu zinaruhusu klabu moja kusajili wachezaji wa kigeni watano, ambapo hakuna kiwango cha kuwatumia kwa pamoja katika mechi ya ligi hiyo.
Wambura amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya kuwepo kwa uvumi kwamba Mabingwa wa Kombe la Kagame Yanga ya jijini Dar es Salaam, inaweza kupokonywa ponti tatu ilizozipata katika mchezo wa juzi dhidi ya JKT Ruvu, baada ya kuwachezesha wachezaji wake wote wa kigeni.

Katika mechi hiyo, Yanga iliwapanga kikosi chwa kwanza wakali wake Mghana Yaw Berko, Didier Kavumbagu wa Burundi, Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite wa Rwanda na Mganda Hamis Kiiza, kabla ya leo asubuhi kuibuka kwa tetesi kuwa Wanajangwani hao watapoteza pointi kwa kuwapanga wote.
“Huo ni uvumi tu, Yanga hawawezi kunyanganywa point zao kwa kuwa hakuna utata wowote wa kuwachezesha wachezaji wa kigeni wote waliosajiliwa ili waisaidie timu kulingana na sheria  za Ligi Kuu,” alisema Wambura.
Wambura alisema kuwa TFF wanakusudia kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni katika Ligi Kuu msimu wa mwaka 2013/14 kutoka wachezaji watano hadi kufikia watatu na si mwaka huu.

No comments:

Post a Comment