Saturday, September 22, 2012

TPBO YAMTEUWA MAHAMOOD SINANI KUWA MAKAMU WA RAIS


Makamu wa kwanza wa Rais wa TPBO MAHAMOOD SINANI
MAHAMOOD SINANI

NINAYO FURAHA KUBWA KUAARFU YAFUATAYO ;-

KATIKA KUIMARISHA SAFU YA UONGOZI WA ORGANAIZESHENI YA NGUMI ZA KULIPWA TANZANIA-TPBO, NIMEAMUWA KUMTEUWA NDG MAHAMOOD SINANI MKAZI WA MKOA WA MTWARA ,KUWA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA TPBO.


UTEUZI WAKE UMANZA   TAREHE 21 -10 -2012 SIKU YA IJUMAA., NA ATAKUWA MAKAMU WA RAIS KWA KIPINDI CHA MIAKA MITATU [3].


IZINGATIWE KWAMBA UTEUZI HUU UMEKWENDA SAMBAMBA KUTOKANA NA SHUGHULI ZA TPBO KUSAMBAA KARIBU MIKOA YOTE YA TANZANIA , HIVYO TUMEONELEA NI BORA TUKAWAPA NAFASI ZA UONGOZI PIA WATU WAISHIO NJE YA DAR-ES-SALAAM ILI WASAIDIANE NASI KUTENGENEZA AJIRA KWA VIJANA WA KITANZANIA KUPITIA NGUMI ZA KULIPWA .

KATIKA UTEUZI HUU PIA KIGEZO CHA ELIMU KIMEZINGATIWA ;-


NDG MAHAMOOD SINANI ANAYO ELIMU IFUATAYO;-

ELIMU YA SECONDARI KUTOKA INTERNATIONAL SHOOL -MOSHI -TANZANIA.

PIA ANAYO DIPLOMA YA BIASHARA ALIYOIPATA KUTOKA CHUO CHA SALISBURY -KILICHOKO NCHINI UINGEREZA.


TPBO INAAMINI KABISA KWAMBA KUTOKANA NA UTEUZI HUU WA NDG MAHAMOOD SINANI SASA MABONDIA WOTE WA NGUMI ZA KULIPWA WA MIKOA YA KUSINI WATAKUWA KATIKA WAKATI MZURI SANA WA KUPATA MAPAMBANO KWANI WAMESHAPATA KIONGOZI AMBAYE KWA KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WENZAKE WA TPBO ATAHAKIKISHA MICHEZO INAANDALIWA MKOANI MTWARA KWA FAIDA YA VIJANA WA MTWARA ILI WAWEZE KUJIAJIRI KUPITIA MICHEZO NA HASA NGUMI ZA KULIPWA.

TPBO INAWAOMBA WAKAZI WA MTWARA NA WADAU WOTE WA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI TANZANIA KUMPA USHIRIKIANO MKUBWA MAKAMU WA RAIS HUYU NDG MAHAMOOD SINANI.


NDG WAANDISHI KWA MAWASILIANO NA MAKAMU HUYU WA RAIS MNAWEZA KUMPATA KWA SIMU  NAMBA  0712-141466

                            IMEANDIKWA NAMI
                      YASSIN ABDALLAH -USTAADH
                            RAIS -TPBO

No comments:

Post a Comment