Wednesday, September 12, 2012

WAANDISHI WA HABARI KILIMANJARO WAKIWA KWENYE MAANDAMANO YA KUMLILIA MWANGOSI



Askari wa Jenshi la Polisi wakilazimika kufanya kazi ya wanahabari kwa kupiga picha
mabango yaliyokuwa yamebebwa na wanahabari hao waliokuwa kwenye maandamano ya kumlilia Mwandishi Mwenzao,Marehemu Daud Mwangosi aliefariki Mkoani Iringa hivi Karibuni.
Wanahabari wa mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika maandamano.
Wanahabari wakiwa na mabango yenye jumbe mbali mbali.
Mwandishi wa habari mkongwe,Nechi Lyimo aliyeketi kwenye pikipiki,jana alilazimika kutoka hosptali alikokuwa akipatiwa matibabu na kuja kuungana na wanahabari wenzake katika maandamano.
Wanahabari wakitoa matamkpo mbamlimbali.Picha na Dixon Busagaga.

RAIS KIKWETE KATIKA ZIARA RASMI YA KISERIKALI (STATE VISIT) YA SIKU TATU NCHINI KENYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mwai E. Kibaki wa Kenya pamoja na ujumbe wake wakiingia Ikulu ya Nairobi Jumanne, 11 Septemba , 2012, alipoanza Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu nchini humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Waziri wa Elimu ya Juu wa Kenya, Mheshimiwa Margaret Kamar alipowasili Chuo Kikuu cha Kenyatta kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo hicho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta. Kulia kwake ni Waziri wa Elimu ya Juu, Mheshimiwa Margaret Kamar na kuhsoto kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Olive Mugendi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi baada ya kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akipozi na wanafunzi wawili waliotoa burudani ya vichekesho wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba ya kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhiwa zawadi ya picha ya kuchora baada ya kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.

No comments:

Post a Comment