Sunday, September 2, 2012

WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI (EALA) KUTOKA TANZANIA WAKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI


 

 
  Mwenyekiti wa Wabunge wa Afrika Mashariki (EALA) Tawi la Tanzania Alhaj Adam Kimbisa (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) na kuviomba vyombo vyao viweze kutambulisha timu ya wabunge hao tisa kwa watanzania ili wapate kuwafahamu kama wawakilishi wao wanaosimamia masuala ya taifa. Kulia ni Mbunge Angela Kizigha ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya biashara na uwekezaji na kamati ya mazingira katika bunge hilo. Picha na Anna Nkinda – Maelezo
 Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Angela Kiziga (kulia) ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya biashara na uwekezaji na kamati ya mazingira akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu tofauti ya kiuchumi na maendeleo baina ya nchi tano wanachama wa jumuia hiyo . Vikao vya Bunge hilo ambavyo ni vya wiki mbili vinatajiwa kuanza kesho jijini Nairobi Nchini Kenya. Kushoto ni Mwenyekiti wa Wabunge hao Alhaj Adam Kimbisa.
  Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Twaha Issa Taslima akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mkataba wa Jumuia ya Afrika Mashariki ambao wataufanyia kazi katika kikao cha Bunge kinachotarajia kuanza kesho mjini Nairobi Nchini Kenya. Wabunge hao waliongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari (Maelezo) uliopo jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa Wabunge wa Afrika Mashariki (EALA) Tawi la Tanzania Shy-Rose Bhanji (kulia) akiongea jambo na Abdullah Mwinyi (kushoto) ambaye ni Mjumbe wa kamati ya mahesabu ya fedha wa bunge hilo wakati wa mkutano baina yao na waandishi wa habari uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam. Vikao vya Bunge hilo ambavyo ni vya wiki mbili vinatajiwa kuanza kesho jijini Nairobi Nchini Kenya
 Mjumbe wa kamati ya mahesabu ya fedha wa bunge la Afrika Mashariki Abdullah Mwinyi akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa uwanja wa Ndege unaoendelea huko Taveta nchini Kenya kwamba hauna dhamira ya kuathiri uwanja wa ndege wa Kilimanjaro. Kulia ni Katibu wa Wabunge hao Tawi la Tanzania Shy-Rose Bhanji .
Kutoka kusho ni Mjumbe wa kamati ya mahesabu ya fedha wa bunge la Afrika Mashariki Abdullah Mwinyi,Katibu wa Wabunge wa Afrika Mashariki (EALA) Tawi la Tanzania Shy-Rose Bhanji, Mwenyekiti wa Wabunge wa Afrika Mashariki (EALA) Tawi la Tanzania Alhaj Adam Kimbisa na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Twaha Issa Taslima
 Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Twaha Issa Taslima akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Katibu wa Wabunge wa Afrika Mashariki (EALA) Tawi la Tanzania Shy-Rose Bhanji (kushoto) akiwaomba waandishi wa habari waweze kutangaza umuhimu wa Bunge hilo na fursa zilizopo kwa wajasiriamali hasa wanawake. Wabunge hao waliongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari (Maelezo) uliopo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti, Alhaj Adam Kimbisa na  Mjumbe wa Kamati ya Mahesabu ya Fedha wa Bunge la Afrika Mashariki, Abdullah Mwinyi.

No comments:

Post a Comment