Sunday, October 28, 2012

ALIKIBA KUMBEBA ABDUKIBA NDANI YA DUNIA






Na Elizabeth John
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Abdukarim Kiba ‘ Abdukiba’ anajipanga kuachia video ya ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Dunia Mapito’, ambao amemshirikisha kaka yake Alikiba.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Abdukiba alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa kazi hiyo ambayo anaamini itafanya vizuri kutokana na uwepo wa kaka yake.

“Kiukweli najisikia furaha sana kuona kazi zangun zinapendwa na mashabiki, na nimeamua kumshirikisha Alikiba kwa kuona kama ni msanii mkubwa na anaelewa anachokifanya katika game,” alisema Abdukiba.

Pia aliwataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kwaajili ya kukipokea kibao hicho, pamoja vinginea ambavyo bado yupo kwenye maandalizi.

Mbali na kibao hicho, Abdukiba alishawahi tamba na vibao vyake kama, Hatuna habari nao, Kizunguzungu, Huyo sio demu na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia hiyo.

No comments:

Post a Comment