Sunday, October 28, 2012

NMB YADHAMINI BONZA LA MICHEZO UDOM



Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Idris Kikula (wa tatu kulia), kwa pamoja na Meneja wa Kanda ya Kati Bi Lilian Mwinula wakisalimia wachezaji wa mpira wa miguu wakati wa bonanza iliyodhaminiwa na NMB iliyofanyika kati ya timu ya wafanyakazi na wanafunzi wa mwaka wa kwanza.
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Shabaan Mlacha akisalimiana na wachezaji wa timu ya mpira wa pete wakati wa bonanza iliyodhaminiwa na Benki ya NMB kati ya timu ya wafanyakazi na wanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni hapo.
 Wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Idris Kikula (wa kwanza kulia) wakati wa bonanza iliyodhaminiwa na Benki ya NMB kati ya timu ya wafanyakazi na wanafunzi wa mwaka wa kwanza.
Meneja wa NMB Kanda ya Kati Bi. Lilian Mwinula (kushoto), akiwa na Meneja wa NMB Idara ya Wateja Binafsi Bw. Abdulmajid Nsekela, Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Idris Kikula na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano Bw. Imani Kajula wakishuhudia michuano hiyo iliyodhaminiwa na Benki ya NMB ikiendelea mkoani Dodoma.

No comments:

Post a Comment