Monday, October 15, 2012

AUDLEY HARRISON ANUSURIKA KIFO ULINGONI


Mashambulizi ya mapema ya David Price (kushoto) kwa Audley Harrison yalianza hivi Ukumbi wa Lecho Arena jijini Liverpool, England jana.
Kisha mashambulizi hayo ya David Price (kulia) yakamlazimisha Audley Harrison (kushoto) kujisalimisha kambani na kuzuia hatari zaidi.
Ndipo makombora mazito mfululizo ya Price, yalimpomzidi uwezo Harrison na kuanguka ulingoni, ambapo hapa mwamuzi anajaribu kumdaka bila mafanikio. Hii ilikuwa ni dakika ya kwanza sekunde ya 22.
 
LIVERPOOL, England
Kwa muda mfupi wa pambano hilo, Harrison alikuwa na kazi moja ya kukwepa makonde mfululizo aliyokuwa akimiminiwa na Price, ingawa mawili mazito yalimpata vema – kabla ya kuanguka na kukimbizwa hospitali akiwa anapumulia mashine
BONDIA Audley Harrison jana Jumamosi amenusurika kifo ulingoni, baada ya kupigwa vibaya katika sekunde ya 82 tangu kuanza kwa pambano lake dhidi ya mpinzani wake David Price aliyekuwa akitetea vema ubingwa wa Uingereza.
Harrison alilazimika kukimbizwa hospitali huku akipumulia mashine, baada ya kukumbana na makombora mazito kwenye Ukumbi wa Echo Arena  jijini Liverpool, kuwania ubingwa wa Uingereza na Jumuiaya ya Madola uzani wa ‘heavyweight.’
Bingwa huyo wa zamani wa Olimpiki, alivunjika pua na kuvuja damu kwa wingi, kabla ya kukimbizwa hospitali kuokoa maisha yake baada ya kufeli kwa huduma za kwanza ulingoni hapo.
Kwa muda mfupi wa pambano hilo, Harrison alikuwa na kazi moja ya kukwepa makonde mfululizo aliyokuwa akimiminiwa na Price, ingawa mawili mazito yalimpata vema – kabla ya kuanguka na kukimbizwa hospitali.
Akizungumzia ushindi wake, Price, 29, aalidai: “Umalizaji wangu pambano ulikuwa mzuri kama nilivyoonesha. Lazima nikiri pia kuwa mimi mwenyewe ilitisha wakati mwingine. Mara baada ya mimi kusikia harufu ya damu, nikajua nimemaliza kazi.
“Nina heshima kubwa sana kwa Audley kutokana na alichowahi kufanya ulingoni. Acha tupate kujua ukweli juu ya hali yake, yeye ni bingwa wa zamani wa Ulaya – ambaye aliwania ubingwa wa dunia dhidi ya David Haye na mimi niko mbali naye.
“Ukweli ni kuwa nina furaha. Najivunia kuwa Mwingereza. Nataka kuhakikisha nchi hii inajivunia pia uwapo wangu kama bondia.”
Ushindi huo wa Price ulikuwa wa 14 katika mapmbano yake, ukiwa ni KO ya 12 na pia ni pambano lake la sita kumshinda mpinzani katika raundi ya kwanza.

No comments:

Post a Comment