Monday, October 15, 2012

BENKI YA CRDB ILIVYOSHIRIKI WIKI YA HUDUMA ZA KIFEDHA


 Baadhi ya Maofisa wa benki ya CRDB
Ofisa Uhusiano wa benki ya CRDB, Nasib Kalamba akifafanua jambo kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Azania, kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo, wakati wa maonesho ya Wiki ya Huduma za Kifedha, yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Picha na Habari Mseto Blog
Baadhi ya wateja wa benki ya CRDB wakiwa katika bandfa la benki hiyo.
Wateja wakipata huduma


Na Mwandishi Wetu

BENKI ya CRDB imeweza  kutoa elimu kwa wajasiriamali katika maonyesho ya uwekezaji yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazimmoja jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika viwanja hivyoAfisa Mikopo wa Wajasurimali wadogo naWakati  Frank Peter alisema kuwa wajasiriamali wanakabiliwa na changamoto za mitaji na kukosa elimu sahihi juu ya kuweza kukopa katika taasisi za fedha.

Alisema kuwa na wajasiriamali wanatakiwa kupata elimu juu ya kuweza kukopa ambapo CRDB inafanya hivyo kutoa elimu mbalimbali  juu ya huduma  ya mikopo.

Alisema kuwa mikopo katika benki hiyo ni kuanzia sh.milioni 1 hadi 500 ambapo dhamana anatakiwa kuwa na mtaji wake kuanzia milioni 3 na kuendelea pamoja na biashara yake kuwa imesajiliwa kupitia mamlaka husika ikiwemo kuwa na utambulisho wa TIN.

Peter alisema katika kutoa mikopo wanaangalia pamoja  na mzunguko wa biashara ya mteja ili kujiridhisha juu ya kuweza kupata mkopo ikiwemo na dhamana ya mali zisizo hamishika na mali nyingi wateja kuwa na nyumba kama sehemu ya dhamna ya mkopo.

Alisema kigezo kingine ni kuangalia umri wa biashara ambao kwa CRDB  ni kuanzia miezi sita  na kuendelea.

No comments:

Post a Comment