Monday, October 1, 2012

BIASHARA YA MAGAZETI YAHUJUMIWA JIJINI DAR. WAUZAJI HUKODISHA MAGAZETI KWA BEI YA TSH 250 HALAFU HUYAFUATA BADALA YA KUYAUZA.


Moja ya maeneo yanapouzwa magazeti jijini Dar es Salaam.              
UCHUNGUZI uliofanywa na blog hii jijini Dar es Salaam hasa maeneo ya Kariakoo kumekuwepo na biashara isiyo ya haki inayofanywa na wauza magazeti ambayo kwakiasi fulani inawahujumu wamiliki wa makampuni hayo.
 Kiutaratibu magazeti yanatakiwa kuuzwa kwa bei halali iliyoandikwa kwenye gazeti na mteja anapaswa kulipia bei hiyo na siyo zaidi na wala pungufu ya bei hiyo. Kilichonisukuma kufanya uchunguzi huo ni pale nilipomuona muuzaji mmoja wa magazeti akipita kuyaacha magazeti kwenye baadhi ya maduka baadaye huyapitia tena na kupewa Tsh250/ tu ikiwa ni malipo kwaajili yakulisoma gazeti hilo.

Raha za Pwani ilikwenda mbali zaidi na kuzungumza na baadhi ya vijana wa mtaa wa Kipata nakunieleza kuwa biashara hiyo ni yakawaida tangu magazeti yalivyopandishwa bei na kuuzwa hadi bei ya Tsh 800.

Mbali na Changamoto ya Mitandao ya Kijamii blogs facebook na mingine mingi bado kunaibuka adui mwengine kwa biashara hiyo ya magazeti hali inayoweza kuhatarisha sekta hiyo mbele ya safari ndefu ya maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

No comments:

Post a Comment