Thursday, October 18, 2012

BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' AJIANDAA KUMKABILI SAIDI MUNDI WA TANGA



IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE'
BONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' mwishoni mwa wiki hii anaingia Kambini kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wake mwingine baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita kumtwanga bondia Jonas Segu wa Dar es salaam

King Class Mawe ataanza mazoezi mwishoni mwa wiki hii kwa ajili ya kumkabiri bondia kutoka Tanga Saidi Mundi mpambano utakaofanyika 9 Desemba katika ukumbi wa PTA Sabasaba

Akizungumza na waandishi wa habari Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema anamuandaa King Class Mawe kwa ajili ya mpambano wake huo kwa kuwa yeye ni mtu wa ushindi kila wakati

Super D alisema bondia wake ataanza mazoezi kwa kuwa mpambano huo ni muhimu kwake kwani kwa sasa ndio kwanza anaonekana katika mapambano makubwa makubwa bondia huyo aliyewai kuwatwanga mabondia wakongwe nchini akiwemo Sako Mwaisege,Jonas Segu aliyemfulumushia kichapo cha paka mwizi na kukubalika kwa mashabiki

Amewaomba wadau mbalimbali kumpa sapoti na kamwe ato waangusha kwa kuwa yeye bila mashabiki na wadau awezi kuwa King amewataka wadau kuendelea kumpa ushirikiano walioutoa wakati wa mpambano wake wa mwisho ili aweze kufika mbali katika anga za masumbwi Duniani

Bondia huyo mwenye kuwa na rekodi ya kupiga wapinzani wake kwa K,O amesema mabondia wa Tanga anawaheshimu sana lakini kwa Said Mundi anataka kutoa mfano ili aweze kuendeleza kuweka jina lake juu katika anga za kimataifa ya mchezo wa Masumbwi

No comments:

Post a Comment