Thursday, October 18, 2012

bondia selemani said galile atakapopambana na mkenya CALED AMAINDA .


tarehe 10 -11-2012 katika uwanja wa mpira wa kinesi ulioko wilaya ya kinondoni kutafanyika pambano lisilo la ubingwa la kimataifa kati ya bondia selemani said galile atakapopambana na mkenya CALED AMAINDA .


PAMBANO HILO LITAKUWA NI LA UZITO WA KILOGRAMMS 72.5 [middle] na litakuwa la raundi 8.



awali selemani galile alikuwa apambane na bondia bingwa wa afrika mashariki na kati THOMAS MASHALI ambaye tayari alikwisha saini mkataba wa pambano hilo ,na kuchukuwa malipo ya awali kutoka kwa promota wa pambano hilo ndg GACHA wa mbega promotion ,hata hivyo imembidi MASHALI kurudisha pesa hizo kwa kuwa amepatwa na maumivu katika pambano lake na mganda medi sebyala lililofanyika hapo tarehe 14-10-2012 katika ukumbi wa friends kona ambapo MASHALI aliibuka mshindi na kutwaka mshindi wa ubingwa wa afrika mashariki na kati.



TPBO inampongeza sana bondia thomas mashali kwa tabia nzuri aliyoonyesha ya kurudisha pesa za awali alizochukuwa kutoka kwa promota GACHA.


kwani siyo rahisi kabisa kuamini kwamba bondia wa tanzania amerudisha pesa alizochukuwa kwa promota ,kwani kumbukumbu zilzopo katika makabrasha ya TPBO ofisini wapo mabondia ambao wamechukuwa pesa za malipo ya awali na wameshakataa kupanda ulingoni kwa visingizio vilivyo nje ya taratibu za ngumi za kulipwa.tena baadhi ya mabondia hao ni wenye majina makubwa sana ktk ngumi za kulipwa.

 imeletwa kwenu nami
yassin abdallah -ustaadh

rais -TPBO

No comments:

Post a Comment