Wednesday, October 17, 2012

KUKAMATWA KWA PONDA KOVA AORODHESHA TUHUMA DHIDIYAKE!



Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalu ya Dar es Salam Suleimani Kova akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu kukamatwa kwa Sheikh Ponda Issa Ponda jana usiku baada ya kuweka mtego kwenye eneo ambalo kwa mujibu wa kova ni mafichoyake na alipelekwa na pikipiki.
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda, wakti akiwahutubiwa waisilamu kwenye maandamano ya hivi karibuni kupinga filamu  iliotengenezwa marekani ya kukashifu mtume kwenye viwanja vya Kidongo Chekundu.
KIONGOZI wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu nchini Sheikh Ponda Issa Ponda ametiwa nguvuni na Jeshi la Polisi jana usiku ambapo kwa mujibu wa Kamanda Kova wamemkamata wakati akienda kwenye mafichoyake muda mfupi tu baada ya kushushwa kwenye pikipiki kwenyeeneo la Chang'ombe jijini Dar es Salaam.

Mbali na kukamatwa Kiongozi huyo pia watu wengine 38 wamekamatwa majira ya saa 4:00 usiku baada ya kufanya operesheni maalum. Watu hao wanakamatwa kwa madaikuwa ni wafuasi wa sheikh Ponda aliongoza kundi hilo kuvamia kiwanja No.311/3/4BLOCK "T"  eneo la Chang'ombe Manispaa ya Temeke.
 Kwenye Taarifa ya Kova kumeelezwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za kusababisha vurugu na vitisho,
Sambamba na hilo Ponda na wafuasi wake anatuhumiwa pia kinume cha sheria walisababisha kuvunjwa kwa makanisa zaidi ya manane siku ya 12/10/2012.

No comments:

Post a Comment