Saturday, October 20, 2012

MTANZANIA RASHID ALLY KUZIPIGA NA MMALAWI WILSON MASAMBA



Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) imetoa kibali kwa bondia Rashid Ally kupiga na Bondia Wilson Masamba pichani wa Malawi katika Motel Paradise jijini Blantyre nchini Malawi 28th October,  2012
 Mpambano huo wa round nane katika uzito waunjoya (featherweight) utakuwa sio wa ubingwa na utakuwa mpambano wa 50 kwa bondia Rashid Ally wakati kwa bondia Wilson Masamba utakuwa mpambano wa 24.
 TPBC inamshauri bondia Rashid Ally ajiandae vizuri ili aweze kupeperusha bendera ya Tanzania vyema nchini Malawi na kuendeleza ushirikiano na urafiki wa nchi hizi mbili.
 Aidha, TPBC inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu mikataba mbalimbali ya ngumi inayotiwa sahihi na mabondia wa kitanzania.
 Mikataba ya ngumi duniani kote hairuhusu kutolewa kwa pesa za maandalizi au awali (advance payment) kwa mabondia wanaopambana.
 Mikataba ya ngumi husainiwa kwa bondia aliyesaini kupewa pesa yake yote baada ya kushuka kwenye ulingo.
 Hizi nisheria za kimataifa na mabondia wanaoendekeza tabia ya kupewa pesa za awali (advance payment) wanapotosha umma na kutia doa tasnia ya ngumi za kulipwa Tanzania.

No comments:

Post a Comment