Saturday, October 20, 2012

TWANGA YAANDAA FACEBOOK FANS PARTY JUMAPILI HII MZALENDO PUB.



WAKALI wa Muziki wa Dansi Bongo African Stars Band “Twanga Pepeta” Jumapili hii 21-10-2012 katika ukumbi wa Mzalendo Pub inatarajia kufanya Patty maalum kwa ajili ya mashabiki wake wa mitandao ya Kijamii (Facebook, Twitter,BBM, Blogs N.k).
Patty hiyo itafanyika katika ukumbi wa Mzalendo Pub uliopo Kijitonyama na matayarisho yote yamekwisha kukamilika na itaanza kuanzia saa tatu usiku mpaka tisa za usiku.
Nia ya kuandaa tafrija ya Twanga facebook Fans Party ni kutambua, kuwathamini na kuwatambua marafiki wote wanaoisapoti Twanga Pepeta kupitia mitandao ya kijamii.
Sambamba na hilo pia Twanga itatumia fursa hiyo kuwathamini wale wote waliotoa mchangu mkubwa (wakiwemo wanamuziki waliopo sasa na waliopita, Vikundi vya mashabiki, Mtu mmoja mmoja, Wanahabari, wanaoendesha Blog mbalimbali, Kumbi mbalimbali , BASATA, Mapromota,  na wengine wote waliotoa sapoti kwa namna moja au nyingine)  kwa kufanikisha mafanikio ya Twanga toka kuanzishwa kwake mpaka leo.
Burudani itatolewa na African Stars Band “Twanga Pepeta” wakishirikiana na baadhi ya wanamuziki waliowahi kuitumikia Twanga Pepeta toka inaanzishwa mpaka leo. Baadhi ya wanamuziki waliothibitisha kushiriki ni Ally Akida, Khalid Chokoraa, Soud Mohammed au MCD na wengine wameahidi kuthibitisha hapo baadae kabla ya kufanyika kwa onyesho.

No comments:

Post a Comment