Thursday, October 11, 2012

NMB YADHAMINI MASHINDANO YA NMB NYERERE MASTER GOLF

 

 Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Kees Verbeek akimkabidhi Mjumbe wa Kamati ya Chama cha Gofu Tanzania (TGU), Meja Samwel Hagu, mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 15 za udhamini wa mashindano ya gofu ya kumbukumbu ya Nyerere 'NMB Nyerere Masters Golf Tournament' katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam leo. Mashindano hayo yatakayoshirikisha wachezaji 100 kutoka mikoa mbalimbali nchini yatafanyika kesho na kesho kutwa kwenye viwanja vya Gymkhana Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa NMB, Josephine Kulwa. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Kees Verbeek akielezea udhamini wao kwenye mashindano hayo.
Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Kees Verbeek akizungumza na Samweli Hagu wa TGU

No comments:

Post a Comment