Wednesday, October 17, 2012

OBAMA AMVUJISHA JASHO ROMNY, KWENYE MDAHALO WA JANA USIKU. AFANYA VIZURI NA KUREJESHA MATUMAINI KWA WAFUASI WAKE.



Wagombea Urais wa Marekani Mitt Romney (kushoto) na Barack Obama wakishambuliana kwenye mdahalo uliofanyika alfajiri ya kuamkia leo majira ya saa 10:00, kwa saa za Afrika Mashariki. Pamoja na wadadisi wa masuala ya kisiasa hawakuridhishwa na kitendo chao cha kuto jibu maswali moja kwamoja badala yake walikua wakishambuliana. 

Mdahalo huo wa pili uliofanyika kwenye Chuo Kikuu cha Hofstra huko Long Island unaonekana kumrejesha kwenye chat Rais Barack Obama, kwa kishindo dhidi ya mpinzani wake wa chama cha Republican Mitt Romney kwa kumfunika

Mdahalo huo wa pili kati ya midahalo mitatu iliyopangwa kufanyika umewapa nguvu wanachama wa Democrats waliokuwa wana hofu baada ya Obama kufanya vibaya kwenye mdahalo wa kwanza wiki mbili zilizopita.

Obama ametetea sera zake na kumchallenge Romney kwa kubadilisha badilisha misimamo kwenye masuala muhimu na kudai kuwa sera za mpinzani wake zitawapendelea matajiri kama akichaguliwa.
Kwa mujibu wa kura za CNN, Obama amefanya vizuri kwa asilimia 46 dhidi ya Romney aliyepata asilimia 39.
Zaidi ya tweets milioni 7 zimeandikwa wakati wa mdahalo huo.

1 comment:

  1. Look At This Site

    Feel free to visit my webpage: attorney lead generation
    Look into my blog post :: seo for attorneys

    ReplyDelete