Friday, October 12, 2012

VILLA SQUAD YAJIANDAA NA LIGI DARAJA LA KWANZA


 Baadhi ya Wachezaji wa Villa Squad wakifanya maxzoezi katika Uwanja wa Kines jijini Dar es Salaam

Kikosi cha timu ya Villa squad Fc wakijifua kwa ajiri ya kujiandaa na ligi ya Taifa daraja la kwanza, inayotarajia kuanza Octoba 20.
kikosi hicho kinajiandaa vizuri mazoezi yake kwenye uwanja wa barafu magomeni. 
akizungumza na mtandao huu, ofisa habari wa villa, Andrew Chale, alisema wachezaji wa hali na morali ya hali ya juu kuakikisha wanarudi ligi kuu ilikuendeleza na ushindani.
"tumedhamiria na tunaweza, villa tupo fiti licha ya changamoto tulizo nazo ila tutapambana mpaka hatua ya mwisho na kurudi ligi kuu msimu ujao".
Chale aliomba mashabiki na wadau wa Villa kujitokeza kwa wingi kwenye mazoezi ya timu hiyo kwenye shule ya Lions Magomeni na kuipa sapoti na kutoa morali zaidi kwa vijana na kuchaingia timu hiyo.
Aidha, Chale alisema kuwa, Ijumaa hii kutakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya COSMOS POLITAN FC ya Kariakoo, mchezo wa kujipima nguvu utakaochezwa uwanja wa makulumla kines

No comments:

Post a Comment