Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, October 15, 2012

Warembo Happiness, Fina waula Tanga Beach Resort


Na  Father Kidevu Blog, Tanga
Warembo wawili wanao wania taji la Redds Miss Tanzania 2012, Happiness Rweyemamu (juu) na Fina Revocatusi, (chini) usiku wa kuammkia leo wamechaguliwa kuwa Mabalozi wa Tanga Beach Resort.

Mabalozi hao walipatakina jana katika shindano dogo la kumsaka Balozi wa Hoteli hiyo ya Kitalii ya jijini Tanga kwa warembo hao kupita mbele ya majaji.

Happiness kutoka Kahama Shinyanga na akiwakilisha Kanda ya Ziwa ndie alishika nafasi ya kwanza na kufuatiwa na Fina ambaye anatoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha na anawakilisha Kanda ya Elimu ya Juujijini Dar es Salaam.

  
FINA REVOCATUS
Akitangaza matokeo hayo Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ndio waandaji wa Miss Tanzania, Hasim Lundenga amesema mbali ya zawadi y ash laki nne kwa mshindi wa kwanza na Laki mbili kwa mshindi wa pili lakini pia warembo hao wamepata ajira Hotelini hapo.

Warembo walio ingia tano bora ni pamoja na Brigitte Alfred wa Sinza, Happiness Rweyemamu, Fina Revocatus, Diana Hussein na Balozi wa Naura Spring Hotel, Eugene Fabian.

Warembo hao wanao wania taji la Redds Miss Tanzania 2012 wamemalizia ziara yao ya kutembeklea vivutia vya utalii Kanda ya Kaskazini jana katika mkoa wa Tanga kwa kutembelea Mapango ya Kale ya Amboni.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...