Monday, October 15, 2012

WASHINDI SITA WA CASTLE LARGER SUPER FANS WAPATIKANA,


Meneja wa bia ya Castle Lager Kabula Nshimo (kushoto) akimkabidhi jezi Denis Mlowe kutoka Iringa ambaye ni miongoni mwa washindi sita wa shindano la kuwasaka mashabiki bomba 2 (Castle Lager Super Fans) watakaoungana na mashabiki wengine wa kinywaji hicho maeneo mbalimbali kwenda kushuhudia fainali za Afrika hapo mwakani nchini Afrika Kusini. Washindi hao watapigiwa kura ili kuwapata wawili watakaowakilisha Tanzania kwenye michuano hiyo.
Kabula akizungumza na waandishi wa habari (hapo pichani) wakati akiwatambulisha washindi hao (kulia) ambao watapigiwa kura ili kuwapata wawili kwenda kuwakilisha Tanzania kwenye kushangilia fainali hizo za Afrika.

Washindi wakiwa na jezi zenye majina yao mara baada ya kutambulishwa mbele ya waandishi wa habari.
Washindi wote kwa majina yao na sehemu wanazotoka ni Stephen Chuma-Dar es Salaam, John Mosha Dar es Salaam, Firbert Nestory Dar es Salaam, Charles Mbaza Arusha, Denis Mlowe na Yahya Hamza

No comments:

Post a Comment