Sunday, October 21, 2012

WASHINDI WA MASHINDANO YA BALIMI KIGOMA WAPATIKANA.


Akina mama wa timu mbalimbali za upigaji wa makasia kwenye mashindano ya mitumbwi ya balimi yaliyofanyika kwenye ziwa Tanganyika Mkoani Kigoma wakichuana vikali kwenye michuano hiyo ambapo timu ya Katonga A kwa upande wa wanaume iliibuka bingwa na kubadhiwa kitita cha Shilingi 900,000 na timu ya Upendo kwa upande wa Wanawake na kukabidhiwa kitita cha Sh 700,000.
WANAUME KAZINI! Miongoni mwa washiriki wa mashindano hayo ya mitumbwi ambao waliingia kwenye tatu bora ya mashindano hayo na kupata nafasi yakwenda kwenye fainali itakayofanyika mwezi Desemba Mkoani Mwanza.

Nahodha wa timu ya upigaji makasia ya Upendo kwenye mashindano ya mitumbwi ya Balimi Bi Mawazo Shabani akipokea kitita cha Tsh 700,000 baada ya kuibuka washindi kwenye mashindano hayo na kupata fursa ya kuwakilisha mkoa huo kwenye fainali itakayofanyika Mkoani Mwanza Desemba mwaka huu.
Mabingwa wa makasia timu ya Katonga A, wakishangilia baada ya kuibuka washindi kwenye mashindano hayo.
Nahodha wa Timu ya Katonga A, akionyesha kitita cha pesa cha Tshilingi 900,000 mara baada ya kukabidhiwa.

No comments:

Post a Comment