Sunday, October 21, 2012

BARABARA YA TOPE KUELEKEA KIGOMA NI KIKWAZO KWA UKUAJI WA UCHUMI WA MKOA

  

Hapa ni kilometa chache tu kutoka Kasulu kuelekea Kigoma Mjini barabara ya tope iliyopata marasha ya mvua inakua kikwazo kwa mabasi hali inayofanya madereva kuachiana kupita kwa zamu kwenye baadhi ya maeneo, mabasi haya yalilazimika kusimama baada ya gari moja la mizigo kunasa kwenye tope hilo.
Baadhi ya watu wakielekea kwenye gari lililonasa kutoa msaada ili liondolewe barabarani hapo na wengine wajaribu bahati yao kama watavuka salama.
Kama ilivyo kwa vijiji vingi nchini magari yanaponasa kwao inakuwa nineema kwa kupata ugeni wasiutarajia kwenye kijiji hichi kilichopo Kasulu pamoja na vijiji bingine vya barabarani nilichoshuhudia watoto wakiomba kutoka kwaabiria ni makopo (chupa tupu za kufadhia maji) nilijaribu kuuliza sana kwanini watoto hao huomba chupa hizo sikupata jibu lakini hali halisi ni hiyo wao wanaomba chupa za maji tu!

No comments:

Post a Comment