Wednesday, October 17, 2012

WASHINDI WA MASHINDANO YA GOFU YA NMB NYERERE MASTERS WAKABIDHIWA ZAWADI





 Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Mark Wiessing akizungumza wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa washindi wa mashindano ya gofu ya NMB Nyerere Masters iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Bodi wa SBL, Jaji mstaafu Mark Bomani akizungumza wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa washindi wa mashindano ya gofu ya NMB Nyerere Masters iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya wachezaji wakiwa katika hafla ya utoaji zawadi kwa washindi
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Mark Wiessing akimkabidhi zawadi mmjoa wa washindi wa mashindano ya gofu ya NMB Nyerere Masters, Jimmy Mollel
 Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa benki ya NMB, Kees Verbeck  akitoa zawadi kwa mmoja wa washindi wa mashindano ya gofu ya NMB Nyerere Masters
 Zawadi
 Baadhi ya zawadi za washindi
 Mshindi wa mashindano ya gofu ya NMB Nyerere Masters, Abdalah Yusuph akivalishwa koti alilokabidhiwa kama zawadi na Mwenyekiti wa Bodi wa SBL, Jaji mstaafu Mark Bomani katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam
 Mshindi wa mashindano ya gofu ya NMB Nyerere Masters, Abdalah Yusuph akiweka sawa koti lake alilokabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya Bia ya Serengeti jaji mstaafu Mark Bomani baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya NMB Nyerere Masters
Mshindi wa mashindano ya gofu ya NMB Nyerere Masters, Abdalah Yusuph akiwa na zawadi zake baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya Bia ya Serengeti jaji mstaafu Mark Bomani (kulia)  katika hafla ya kutoa zawadi iliyofanyika katika Viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam
 Washindi wa mashindano ya gofu ya NMB Nyerere Masters wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi pamoja na maofisa wa benki ya NMB ambao ndio waliodhamini mashindano hayo ya kumbukumbu ya Mwalimu
Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya Bia ya Serengeti jaji mstaafu Mark Bomani (kulia) akimkabidhi mshindi wa mashindano ya gofu ya NMB Nyerere Masters, Abdalah Yusuph (kushoto) katika hafla ya kutoa zawadi iliyofanyika katika Viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa benki ya NMB, Kees Verbeck na Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Mark Wiessing (nyuma aliyenyoosha mkono)

Na Mwamdishi Maalum
Mchezaji Abdalah Yusuph juzi aliweza kuwa mshindi wa mashindano ya ya golf ya NMB Nyerere Master baada ya kushinda kwa mikwaju ya net 137 katika mashindano yaliyofanyika katika viwanja vya Dsm gymkhana.
Mashindano hayo yaliweza kushirikisha wachezaji zaidi ya 100 kutoka katika vilabu vya Lugalo,Tpc,Moshi,Arusha gymkhana,Morogoro ,Kenya na wenyeji Dsm gymkhana.
Kwa upande wanawake mshindi alikuwa Young Suk Choi ambaye aliweza kushinda kwa mikwaju ya netti 137 na nafasi ya pili ikaenda kwa Amina Khamisi aliyepata netti 139.
Kwa upande wa divion B mshindi alikuwa Vikasi Valma  aliyeshinda kwa mikwaju ya netti 135,na nafasi ya pili ikaenda kwa Salumu iddy aliyepata netti 135
Katika mashindano hayo ya NMB Nyerere Master kulikuwepo na mashindano ya golf ya kulipwa ambapo Hassan Kadio aliweza kushinda kwa mikwaju ya gross 135.
Nafasi ya pili ilikwenda kwa Yassini Salehe ambaye aliweza kupiga mikwaju ya gross 143,siku ya kwanza mchezaji huo aliweza kupata gross 69 siku ya pili akapata gross 74.
Wachezaji wengine Fadhiri Nkya aliweza kupata gross 146,Salimu Mwanyenza gross 149 Jeofery Leveriani gross 150 wote kutoka Dsm gymkhan.
Wengine John Davids kutoka klabu ya Lessure [Mombasa] gross 153,Rajabu Iddi gross 157 Mbwana juma gross 157,Brayson Nyenza gross 164,Daudi Helela [Lugalo] gross 164 na Salimu Dilunga gross 175 wote kutoka Dsm gymkhana.
Mashindano hayo ya golf yaliandaliwa kwa ajili ya kumuenzi baba wa Taifa mwalimu julias Kambarage Nyerere aliyefariki miaka 13 iliyopita na yaliandaliwa  na chama cha mchezo wa golf nchini [Tgu] yakiwa chini ya udhamini wa benki ya NMB

No comments:

Post a Comment