Tuesday, November 13, 2012

ANDY MURRAY ATAMBIA MAFANIKIO YAKE 2012




LONDON, England
Wakati akitambia kile alichofanya mwaka huu, Murray ‘Muzza,’ hakusita kusifu kiwango cha mpinzani wake Roger Federer, ambaye alimng’oa katika fainali za ATP kwa seti mbili za 7-6 6-2 na kutinga fainali alikoumana jana na Novak Djokovic.
NYOTA wa tenisi duniani, Andy Murray (pichani juu/kulia), amejipongeza kwa mng’aro aliopata mwaka huu, katika tasnia ya mchezo huo.
Tambo za kinara huyo wa tenisi Uingereza, zimekuja wakati akishindwa kuwika katika fainali za dunia za ATP World Tour, akitambia mafanikio yake katika mashindano ya Olimpiki na ubingwa wa michuano ya wazi ya Marekani ‘US Open.’
Wakati akitambia alichofanya mwaka huu, Murray ‘Muzza,’ hakusita kusifu kiwango cha mpinzani wake Roger Federer, ambaye alimng’oa katika fainali za ATP kwa seti mbili za 7-6 6-2 na kutinga fainali alikoumana jana na Novak Djokovic.
Murray akafunguka akisema: “Federer alicheza vema. Mimi nilianza vizuri, kisha naye akaja vema na kushinda mchezo.
“Ni vigumu sana kumzuia wakati anapokuwa amekutangulia na kimsingi nilimpa faida kubwa na ikawa ngumu kwangu kurejea uongozi.
“Ningefurahishwa kama ningefanikiwa kumakliza mwaka huu kwa kutwaa ubingwa wa fainali hizi tukuka.
“Lakini kwangu mimi ulikuwa ni mwaka bora kulinganisha na mingine katika kipindi kilichopita cha uchezaji tenisi kilicho na umbali mrefu. Naangalia nyuma kwa mtazamo chanya, nikiamini sikukosea pakubwa sana.”

No comments:

Post a Comment