Tuesday, November 13, 2012

AIRTEL DIVA yatoa msaada kwa Wodi ya Watoto wanaougua maradhi ya Kansa Hospitali ya Taifa Muhimbili


Mkurugenzi wa Mawasaliano wa Airtel, Bi Beatrice Singano  Mallya(kulia)  akikabidhi  computer kwa  Mkuu wa kitengo cha wodi ya watoto wanaougua Saratani  kwa Daktari Sulende Kubhodja  wa  hospitali ya Muhimbili , (kati ni) meneja wa jengo la wodi hiyo sista Judica  Mwambo. Wafanyakazi wanawake wa Airtel Tanzania  walitembelea hospitalini hapo  mwishoni mwa wiki hii na kujitolea pia vifaa mbalimbali vikiwemo vitendea kazi vitakavyotumika kafanya usafi kwa wagonjwa  waliolazwa hospitalini hapo Muhimbili.

Wafanyakazi wanawake wa Airtel (Airtel Divas) wakikaribishwa na Meneja wa wodi ya watoto wanaougua Saratani katika Hospitali ya Muhimbili sista Judica Mwambo ambapo hao walitembelea hospitalini hapo  mwishoni mwa wiki hii na kujitolea pia vifaa mbalimbali vikiwemo vitendea kazi vitakavyotumika kafanya usafi kwa wagonjwa  waliolazwa hospitalini hapo Muhimbili.

Mkurugenzi wa Mawasaliano wa Airtel bi Beatrice Singano Mallya (wapili kulia)akiongea na mmoja wa watoto  waiolazwa katika hospitali ya Muhimbili mwishoni mwa wiki hii ambapo wafanyakazi  wanawake wa Airtel waliamua kutembea watoto wenye kuugua Saratani katika Hospitali hiyo mwishoni mwa wiki hii, akifuwatiwa na Afisa uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde. Airtel ilijitolea vitu mbalimabli kwaajili ya hospitali hiyo ikiwemo computer, pamoja sabuni, miswaki, na dawa za meno kwaajili ya wagonjwa hao.

Wafanyakazi wanawake wa Airtel (Airtel Divas) wakiingia na mizigo yao katika wodi wa wagonjwa wanasumbuliwa na maradhi ya  Saratani katika Hospitali ya Muhimbili, wafanyakazi hao walitembelea hospitalini hapo mwishoni mwa wiki hii na kujitolea pia vifaa mbalimbali vikiwemo vitendea kazi vitakavyotumika kafanya usafi kwa wagonjwa  waliolazwa hospitalini hapo Muhimbili

*************
Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel  kupitia programu yake ya AIRTEL DIVA imekabidhi misaada mbalimbali kwa wodi ya Watoto wanaougua maradhi ya Kansa katika Hospital ya Taifa Muhimbili. Ikiwa ni mchango toka kwa wafanyakazi wanawake wa Airtel kuunga mkono jitihada za
Airtel katika kujitolea kwa jamii.

Vifaa vilivokabidhiwa na wanafanyakazi hao wanawake wa Airtel Diva’s ni pamoja ma Kompyuta mpya kwaajili ya wodi hiyo, itakayotumika kutunza kumbukumbu za wagonjwa, pamoja na vifaa mbalimbali vikiwemo vitendea kazi vitakavyotumika katika usafi kwa wagonjwa  waliolazwa hospitalini hapo Muhimbili

Akizungumza Katika wakati wa kukabidhi Misaada hiyo,Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano,amesema kuwa  utoaji misaada hiyo ni Mikakati thabiti iliyowekwa na kampuni hiyo katika kuhakikisha inakuwa karibu zaidi na jamii, sambamba na kutambua mchango wao katika
kufanikisha jukumu zima la Biashara katika kipindi cha Mwaka mzima.

Singano amesema kuwa AIRTEL inatambua changamoto mbalimbali zinazoikabili Wodi ya Watoto wanaougua maradhi ya Kansa,na kubainisha kuwa Msaada walioutoa hautaishia hapo badala yake watakuwa wakifanya hivyo mara kwa mara katika Hospitali mbalimbali za ndani na nje ya Mkoa wa Dar es Salaam.

 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrice Singano  alisema Airtel kupitia mpango wao wa Diva,  unaoundwa na wafanyakazi wote wanawake waliona ni vyema kusaidiana na wazazi wenzao kwa kuwapa pole.
 "Msaada huu tunaokabidhi leo tunaamini utagusa pia wadau wengine kuja kuwatembelea watoto na ndugu zetu wanaugua maradhi ya kansa katika hospital ya Muhimbili na hata zingine kwa lengo la kusaidiana Tumejionea wenyewe shida wanazopata ndugu zetu na hata wauguzaji hivyo tunaomba sana wanaweza kujitolea kuja kwa wingi na kuhakikisha tunasaidiana kwa hali na mali kunusuru maisha ya ndugu zetu hawa”alisema Bi Singano.

 Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Watoto kutoka Hospital ya Taifa Muhimbili DOKTA SURENDE KUBOJA, ameishukuru Kampuni ya AIRTEL kwa msaada walioutoa katika Wodi hiyo na kuyataka Makampuni mengine ya Kibiashara kuiga mfano uliuoonyeshwa na AIRTEL.

Naye Meneja wa Jengo la Watoto kutoka Hospitalini hapo Bi JULITHA MBWAMBO amesema kuwa Watoto wanaotibiwa katika Wodi hiyo wamekuwa wakikabiliwa na Changamoto mbalimbali hivyo Misaada iliyotolewa na AIRTEL itawasaidia katika kupunguza matatizo mbalimbali yanayowakabili.

Nao baadhi ya Wazazi waliozungumza wodini hapo wamesema kuwa Watoto wanaowauguza wanahitaji faraja zaidi katika Maisha yao na kuyaomba makampuni mbalimbali kufuata nyayo za Airtel kwa kuwatembelea na kuwafariji zaidi.

Pia ZUWENA LISELE Mzazi anayeuguza nae alisema “maisha ya hospitali ukiwa unauguza ni magumu sana kwa kuwa hakuna anaekuwa amejipanga kwaajili ya kukabiliana na changamoto za ugonjwa kwa wakati unapotokea , hivyo kwa niaba ya wenzangu wote ninawashukuru sana wanawake wenzagu kutoka Airtel kwa kuliona hili na kuja kutoa pole hii, kwa kweli tumefarijika.

Airtel Diva ni mpango ulio chini ya wafanyakazi wote wanawake wa Airtel Tanzania wenye lengo la kuwaweka  pamoja kujadili changamoto mbalimbali za kijamii na kuzitolea ufumbuzi kwa lengo la kuimarishana.

Airtel Diva pia wanalengo la kuhakikisha wanatoka nje ya mazingira ya kazi na kuhudumia jamii kwa hali na mali ili kutatua changamoto mbalimbali zikiwemo kuchangia Afya, pamoja na kuelimisha moto wa kike na jamii kwa ujumla kutambua haki zao.

No comments:

Post a Comment