Monday, November 12, 2012

ASHANTI HAIKAMATIKI LIGI DARAJA LA KWANZA, YAIGARAGAZA VILLA SQUAD KARUME 2.0


Mchezaji wa Ashanti akijaribu kumtoka beki wa Villa wakati wa mchezo uliochezwa leo uwanja wa Karume


Wachezaji wa Ashanti wakishangilia bao la pili

Mnanda na mdundiko uliamua kuingia uwanjani baadaa ya mchezo kumalizika, huku golikipa wa Ashanti akishindwa kujizuia akaanza kuyarudi

Mashabiki wakambeba kutokana na kazi yake kubwa aliyoifanya ya kupangua mashuti makali

TIMU ya Ashanti aka watoto wa mjini leo wameichapa bila huruma Villa Squad mabao 2-0 kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa uwanja wa Karume, jijini Dar es salaam.

Ashanti walipata bao la kwanza dakika ya nne kupitia kwa Jerome Lembeli bao lililodumu kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza.


Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambuliana lakini Villa watajutia nafasi za wazi tatu ambazo mashuti yalitoka nje kutokana na washambuliaji kutokuwa makini.


Dakika ya 88 Jerome Lembeli tena aliahamsha ramsharamsha za kidedea na mnanda uliokuwa unapigwa nje ya uzio wa uwanja wa Karume baada ya kufunga bao la pili lililozima matumaini ya kusawazisha.


Dakika ya 59 Villa Squad walipata pigo baada ya mchezaji Raymond Zablon kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea kwa makusudi tena mchezo ukiwa haupo mchezoni mhezaji wa Ashanti United.


Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani Wanajeshi wa JW Green Warriors waliwachezesha kwata wenzao Transit Camp kwa kuifunga bao 1-0.

 Bao pekee hilo lilitiwa kimiani na  Zamkufo Elius  dakika ya 40

Kwa matokeo haya Ashanti inaendelea kuongoza kundi B baada ya kucheza michezo mitano na kufikisha pointi 15


Kundi A, Mjini Iringa Polisi Iringa wameifunga Burkina Fasso ya Morogoro mabao 2-0.

Mabao yamefungwa na Dimosi Malisa dakika ya 53 na Japhet Mamboleo dakika ya 57.



Timu ya Ashanti mbali na kutamba katika soka pia inatamba katika timu ya masumbwi chini ya kocha wa kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D'

No comments:

Post a Comment