Tuesday, November 13, 2012

HARAMBEE STARS WATUA MWANZA KUIVAA TAIFA STARS



 Kikosi cha Harambee Stars katika picha ya pamoja
Mshambuliaji Victor Wanyama akiwa na mlinda mlango wa Harambee Stars Arnold Origi, ambao wanasadikika kuwa hawatocheza pambano dhidi ya Taifa Stars, licha ya kutua nchini leo na timu yao.
 
Na Irene Mark
Nao wachezaji wa Yanga waliokuwa na klabu yao jijini Tanga kwa ajili ya pambano lao dhidi ya Coastal Union, wamewasili jijini humo jana mchana, tayari kwa mechi hiyo itakayopigwa kesho saa 10:00 alasiri
KIKOSI cha wachezaji 23 na viongozi 10 wa timu ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars,’ kimetua jijini Mwanza leo saa 2:30 asubuhi, kwa ajili ya pambano la kimataifa la kirafiki, dhidi ya wenyeji Taifa Stars litakalofanyika kesho Jumatano kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.
Habari zilizoifikia Habari Mseto kutoka jijini humo zinapasha kuwa, Harambee Stars imewasili kwa ndege ya Precision na kushukia kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza tayari kwa mtanange huo, huku ikidaiwa kuwa nyota wake wawili hawatocheza pambano hilo, licha ya kutua nchini na kikosi chao.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, nyota wa Celtic ya Uskochi, Victor Wanyama aliyefunga bao la kwanza katika ushindi wa mabao 2-1 wa Celtic dhidi ya FC Barcelona ya Hispania, ni miongoni mwa nyota wa kulipwa walioambatana na kikosi hicho, ingawa inadawa hatocheza sambamba na kipa Arnold Otieno.
chanzo chetu kiewataja wachezaji waliotua na kikosi hicho kuwa ni Arnold Otieno, Dennis Oliech, Victor Wanyama, Ayub Masika, Brian Onyango, Patrick Oboya na Patrick Osiako, Jerry Santo na Fredrick Onyango.
Wengine waliomo kwenye kikosi hicho ni Edwin Wafula, Eugene Asike, Geofrey Odhiambo, Mulinge Ndeto, Christopher Nyangweso, James Situma, Peter Opiyo, Charles Okwemba, Francis Wambura, Andrew Tololwa, Osborne Monday, Wesley Kemboi na Moses Arita.
Viongozi watakaoambatana na kikosi hicho ni pamoja na Kocha Henry Michel, anayesaidiwa na Mohammed Boujarari, huku viongozi wengine wakiwa ni Florent Louis Robert Motta, Sunil Shah, Wycliff Makanga, Wilberforce Juma, Benson Otieno, Ali Rehan, Robert Akumu na Angeline Nzavi.
Aidha, Osiah aliongeza kuwa, wachezaji wa Yanga waliokuwa na klabu yao jijini Tanga kwa ajili ya pambano lao dhidi ya Coastal Union, Frank Domayo, Simon Msuva na Athuman Chuji na Kelvin Yondani, wamewasili jijini Mwanza jana mchana, tayari kwa mechi hiyo itakayopigwa kesho saa 10:00 alasiri.
Osiah alimaliza kwa kutaja viingilio vya mechi hiyo, ambapo alisema vitakuwa ni shilingi 15,000 kwa watazamaji wa Jukwaa Kuu, huku wale wa mzunguko wakitakiwa kulipa shilingi 5,000 kuliona pambano hilo lililo kwenye kalenda ya Fifa.

No comments:

Post a Comment