Monday, November 26, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAHUTUBIA WANANCHI WA MKOA MPYA WA KATAVI WAKATI AKIZINDUA MKOA HUO JANA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Mkoa mpya wa Katavi, wakati wa sherehe za uzinduzi wa mkoa huo mpya zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kashaulili mkoani Katavi jana Nov 25, 2012.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi rasmi wa Mkoa mpya wa Katavi, wakati wa sherehe za uzinduzi wa mkoa huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kashaulili, mkoani Katavi jana Nov 25, 2012.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Majaribio wa Kampuni ya CAMARIEC, Eng. Wilson Baitani, kuhusu utengenezaji wa Mashine ya gharama nafuu ya kukamulia asali, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika kilele cha sherehe za uzinduzi wa mkoa wa Katavi, jana Nov 25, 2012 mkoani Katavi. Wa pili (kushoto) ni mke wa Makamu, Mama Zakhia Bilal.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Kikombe cha mshindi wa pili katika mashindano rasmi ya sherehe za uzinduzi wa Mkoa mpya wa Katavi, Nahodha wa timu ya Polisi ya Netiboli mkoa wa Katavi, Lawrensea Sanga, wakati wa sherehe hizo za uzinduzi zilizofikia kilele jana Nov 25, 2012 katika Uwanja wa Kashaulili, mkoani Katavi.
 Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakizungumza na Mbunge wa Mpanda, Zalafi, kupitia CUF, wakati Makamu akiondoka katika Uwanja wa Kashaulili baada ya kuwahutubia wananchi, jana.

Mwanamuziki Hamza Kalala na kundi lake la Wanakasimbagu, wakitoa burudani wakati wa sherehe za uzinduzi huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kashaulili mkoani Katavi, jana.

No comments:

Post a Comment