Monday, November 26, 2012

ZIARA YA DK.SHEIN NCHINI VIETNAM YAENDELEA.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, na  Mkurugenzi wa Chuo cha Taasisi ya utafiti wa Sayansi ya kilimo nchini Vietnam,(Vietnam Academy of Agricultural Sciennces (VAAS), Dr.Phan Thi Van, (katikati) wakipanda mti baada ya kupata  taarifa za Tafiti za ufugaji wa Samaki zilizotolewa na Mkurugenzi huyo, wakati wa ziara ya Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ulipotembelea katika Taasisi hiyo nchini Vietnam,ikionesha ishara ya uhusiano na ushirikiano kwa nchi hizo 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiagana na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dr.Phan Thi Van,(kulia)baada ya kupiga picha ya pamoja baada ya kupata  taarifa za Tafiti za ufugaji wa Samaki zilizotolewa na Mkurugenzi huyo,wakati wa ziara ya Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,ulipotembelea katika Taasisi hiyo nchini Vietnam
Baadhi ya maafisa walio katika ujumbe wa ziara ya Rais wa Zanzib ar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein nchini Vietnam,wakisikiliza kwa makini taarifa za tafiti mbali mbali za Taasisi ya ufugaji wa Samaki ,zilizotolewa na Mkurugenzi Dr.Phan Thi Van,wakati ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,ulipofanya ziara kutembelea kituo cha utafiti huo nchini Vietnam.

No comments:

Post a Comment