Monday, November 26, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA UWANJA WA NDEGE WA MPANDA MKOA MPYA WA KATAVI


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, wakati wa hafla ya uzinduzi wa uwanja huo iliyofanyika mkoa Mpya wa Katavi, leo katika uwanja huo baada ya kukamilika kwa ukarabati uliogharimu kiasi cha Sh. Bilioni 30. Kulia ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, (kushoto) ni Mama Zakhia Bilal (wa pili kushoto) ni Katibu Mkuu wa Miundombinu, Omar Chombo na  Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt.Charles Tizeba. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuweka jiwe la msingi, kuashiria uzinduzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, uliopo Mkoani Katavi. Uzinduzi huo umefanyika leo katika uwanja huo uliopo Mkoa wa Katavi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili ya kikundi cha sanaa cha Hiyari ya Moyo chenye maskani yake, Mpanda mjini, wakati walipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mpanda, leo kwa ajili ya kuzindua rasmi uwanja huo na Mkoa wa Katavi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili ya kikundi cha sanaa cha Mama Monica, chenye maskani yake, Maji Moto Mpanda mjini, wakati walipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mpanda, leo kwa ajili ya kuzindua rasmi uwanja huo na Mkoa wa Katavi.
Mbunge mstaafu, Chrisant Mzindakaya, akijumuika na wasanii wa ngoza ya asili kucheza ngoma ya kabila la Wakonongo wa Inyonga, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, uliofanyika sambamba na uzinduzi wa mkoa mpya wa Katavi.

No comments:

Post a Comment