Friday, November 23, 2012

TIGO YASHIKA NAFASI YA 5 KWA UBORA WA KUTOA HUDUMA KWA MITANDAO YA KIJAMII


Tigo yashika nafasi ya 5 duniani na ya kwanza Afrika kwa makampuni ya simu katika  kujitoa kwa huduma za mitandao ya kijamii, hii ni kulingana na matokeo yaliyotolewa jana na kampuni  ya ‘Socialbakers’ inayohusika na masoko, ufuatiliaji na upimaji wa mitandao ya kijamii duniani. 
Tigo Tanzania ina wastani wa kujibu wa dakika 24 na kiwango cha majibu ya 87.49% dhidi ya kiwango cha dakika 520 na kiwango cha 65.50% kiwango cha kujibu, kwa sekta hii. Makampuni au bidhaa ambazo zinajitoa kwa huduma bora za mitandao ya kijamii zinaonekana kuwa na huduma bora kwa wateja.
“Tunajivunia  kuweza kushika namba 5 bora kwa operasheni zetu duniani na kuwa bora zaidi kwa Afrika.Hili inaonyesha wazi  juhudi na nguvu tunazoweka ili kuhakikisha kuwa tunaongea na kuwasikiliza wateja wetu wakati wote, kwa njia inayokwenda na wakati wa sasa, alisema, Diego Gutierrez Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Tigo Tanzania”.
Huduma za kijamii kwa wateja na vipimo vyake ni pamoja na idadi ya mashabiki,idadi ya maswali yanayoulizwa na mashabiki wa kurasa,muda wa majibu,wastani wa muda ambao kampuni inachukua kujibu maandiko ya watumaji na kiwango cha majibu au asilimia ya wanaopata majibu kutoka kampuni hiyo.
Kwa sasa Tigo Tanzania imefikisha mashabiki 110,000 wa Facebook na kuwa mtandao unaoongoza kwa kuwa na wafuasi wengi facebook.
Socialbakers ni moja kati ya kampuni kubwa zinazofanya tathmini ya mitandao ya kijamii duniani na lengo lake kubwa ni kufuatilia na kupima muonekano ya mitandao, katika kila lengo la mtandao dunia nzima pale ilipo. Socialbakers pia ni moja kati ya kampuni za kuendeleza masoko zinazotumiwa na Facebook .

No comments:

Post a Comment