Friday, November 16, 2012

MWAKAREBELA USO KWA USO NA BAYI



Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela amejitosa kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya kuwa Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) ambayo pia inawaniwa na katibu mkuu wa sasa, Filbert Bayi.

Mwakalebela ambaye aliondoka TFF baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka miwili na kwenda kuwania ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambako hakufanikiwa baada ya kuenguliwa na chama chake, atachuana pia kuwania kugombea nafasi hiyo na mwanariadha nyota wa zamani nchini, Juma Ikangaa.
Wengine waliojitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa TOC utakaofanyika Desemba 8 mkoani Dodoma ni Jackson Kalikuntima, Saadun Ahmed Khamis, Abdulhakim, Henry Tandau na Hassan Jarufu wanaowania kugombea nafasi ya makamu wa rais wa kamati hiyo.

 , Afisa Michezo wa TOC, Mwinga Mwanjala aliwataja waliojitokeza kuchuku fomu kuwania ujumbe ni Michael Changarawe, Noel Kiunsi, Irene Mwakasanga na rais wa Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui.

Wengine wanaowania ujumbe ni Muharami Mchume, Noorelain Shariff, Lina Paul Kessy, Vitalis Kulindwa Shija, Salum Salum, Peter Mwita, Zakaria Gwandu, Mwera Samwel, Jamal Nassor Adi, Haudface Rwegeshora na Khamis Gulam,
Wanamichezo zaidi waliojitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi mbalimbali ni Charlse Nyange (Mhazini) na wanaowania nafasi ya katibu mkuu msaidizi ambao ni David Mwakiposa, Fabiano Naasi, Nassra Juma Mohamed, Suleiman Khamis, Suleiman Mahamoud na Abdlrahman Hassan.

Wanaowania urais wa TOC ni rais wa sasa, Gullam Rashid na Khamis Abdallah Said, wakati Juma Khamis Zaidy wanawania nafasi ya kuwa mhazini mkuu msaidizi.

Mwanjala alisema kuwa mwisho wa kuchukua ulitarajiwa kuwa jana jioni na usaili utafanyika Novemba 20 na mwingine utafanyika Zanzibar Novemba 24.

Alisema kabla ya uchaguzi mkuu kutakuwa na mkutano mkuu wa uchaguzi ambao umepangwa kufanyika Desemba 6 mkoani Dodoma, ukifuatiwa na uchaguzi wa kamisheni ya wachezaji ambayo nayo itachaguliwa siku hiyo ya mkutano mkuu.

Wakati huo huo, kamati ya TOC itakutana kesho visiwani Zanzibar kupanga mikakati ya kufanikisha uchaguzi mkuu.

No comments:

Post a Comment