Thursday, November 8, 2012

TAARRIFA ZA WATU KUGANDANA JIJINI DAR SIO ZA KWELI, Mganga Mkuu Temeke azungumza na Raha za Pwani. Hospitalini Temeke kwafurika wat, mabomu yapigwa.



WAKATI taarifa za watu wawili mwanamke na mwanaume waliokuwa wakifanya ngono kuzidi kusambaa taarifa kutoka Hospitali ya temeke zinaeleza kuwa mabomu  yamepigwa kutawanya watu baada ya watu kujazana Hospitalini hapa kufuatilia tukio hilo.
Taarifa hizo ambazo zimekua ni gumzo mchana kutwa waleo zinaeleza kuwa watu hao wametolewa ndani ya guest fulani maeneo ya mtoni kwa Azizi Ally  wakiwa wanavunja amri ya sita ya mungu ambapo imeelezwa mwanamke ni mke wa mtu na mwanaume pia ni mume wa mtu. 
Hadi blog hii inaripoti taarifa hizi imeelezwa kuwa tayari mke wa mtu huyo ameshafariki kwa presha na marehemu pamoja na mume wa mtu wote wamepelekwa mochwari wakati wakitafakari nini kifanyike.
Akizungumza na Blog hii kwa njia ya simu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke Amani Malima amekanusha vikali kuwepo kwa tukio hilo huku akionyesha kushangazwa taarifa hizo. 
"Ndugu Mwandishi hapa sisi tumesitisha huduma kabisa kwa muda huu hatuwezi kuendelea kutoa huduma kwa mazira haya na taarifa hizo sio sahihi sijui ninani anaeneza uvumi huo" Alisema Malima. Kwa siku nzima ya leo kwenye mitandao ya kijamii kumekuwa na gumzo kubwa kuhusu tujio hilo huku zikisambazwa picha ambazo blog hii imezipost lakini haina uhakika kama nikweli picha za watu hao.
Kutokana na eneo la Hospitali kuwekwa ulinzi mkali muda wajioni tumeshindwa kuwaletea picha za matukio yanayoendelea Hospitalini hapo.

No comments:

Post a Comment