Mwakilishi wa taasisi ya Molly’s inayojihusisha na utoaji
misaada kwa taasisi za kijamii Catharine Paul Hiicks (watatu kushoto)
akimkabidhi cheki yenye thamani ya Dola
za kimarekani 2369/ Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Saratani ya Matiti Tanzania
Angela Kuzilwa, mara baada ya kukabidhi msaada wa matiti bandia na sidiria
maalum kwaajili ya waliokatwa matiti vyenye thamani ya zaidi ya Tsh 10Millioni
jijini Dar es Salaam leo.
Wafanyakazi wa Asasi ya Saratani ya Matiti Tanzania na
baadhi ya wanachama wa taasisi hiyo wakiinua juu moja ya maboksi yenye matiti
bandia na sidiria maalum kwaajili ya watu waliokatwa matiti mara baada ya
kukabidhiwa na Mwakilishi wa Taasisi ya Molly’s Catharine Paul Hicks vyenye
thamani ya zaidi ya Dola 10Millioni jijini Dar es Salaam leo.
"Ni siku ya furaha sana kwetu leo" |
"Ahsante kwa msaada Tunashukuru" |
ASASI ya Saratani
ya Matiti Tanzania leo imepokea Msaada
wa matiti bandia na sidiria maalum kwaajili ya waliokatwa matiti pamoja
na msaada wa cheki ya pesa , vyenye
thamani ya zaidi ya Millioni 12.
Akizungumza na Mtandao huu mara baada ya kukabidhiwa vifaa
hivyo na Cheki Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Angela Kuzilwa, alisema wamekabidhiwa
msaada wa matiti bandia yapatayo 30 na sidiria maalumu zipatazo 30, pamoja na
Cheki yenye thamani ya Dola za Kimarekani 2369 kutoka kwa taasisi ya Molly’s
inayojihusisha na utoaji wa misada ya kjamii.
Kuzilwa aliuambia mtandao huu kuwa wamekua na changamoto
nyingi kwenye taasisi hiyo ambazo pekeyao hawataweza kuzikabili bila kupata misaada kutoka kwa taasisi na
mashirika mbalimbali pamoja na Serikali.
Pamoja na kuishukuru taasisi ya Molly’s Kuzilwa amesema
vifaa bandia kwa waathirika wasaratani ni ghali sana kiasi kwamba mtanzania
wakawaida ni vigumu kuweza kumudu kununua ambapo alitoa mfano wa titi moja
bandia linafikia thamani ya Tsh 300,000/ (laki tatu).
Nae mwakilishi wa Taasisi ya Molly’s alisema taasisi yao
iliwatembelea na kuzungumza nao viongozi wa taasisi hiyo ilikujua Changamoto
zinazowakabili ndipo walipogundua tatizo hilo na kuwatafutia fedha za kununua
vifaa hivyo kutoka kwa wahisani wengini nchini Uingereza.
Asasi ya Saratani Tanzania ilianzishwa mwaka 2008 ili kuweza
kuunganisha nguvu kwa walioathirika saratani na kuweza kuweza kuwasaidia wengine
wanahisi dalili zakuwa na saratani ambapo hadi hivio sasa wanawanachama zaidi
ya 370.
No comments:
Post a Comment