Tuesday, December 18, 2012

WANAWAKE WAJASIRIAMALI WA KATA YA KIPAWA WAPATA MAFUNZO YA UFUNDI STADI NA UJASIRIAMALI



Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dk.Makongoro Mahanga akifungua Mafunzo ya Wanawake Wajasiriamali wa Kata ya Kipawa Manispaa ya Ilala Dar es Salaam leo. Kushoto ni Msaidizi wa Waziri Mohamed Michuzi, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kipawa Said Fundi na Diwani wa Kata hiyo Bonnah Kaluwa.
Wakina mama wajasiriamali wakiwa katika mafunzo hayo
Wanawake Wajasiriamali wakisubiri kuingia katika mafunzo hayo

Na Dotto Mwaibale
NAIBU Waziri wa Kazi na Ajira Dk.Makongoro Mahanga amesema ukosefu wa ajira hapa nchini ni jambo tete ambapo kila mtu anatakiwa kujiajiri mwenyewe ili kukabiliana na sua hilo.
Hayo aliyasema wakati akifungua mafunzo ya ufundi stadi na ujasiriamali kwa wanawake wa Kata ya Kipawa Dar es Salaam leo.
Alisema suala la upatikanaji wa ajiri haipaswi kuachiwa kwa serikali pekee bali kila mtu mmoja mmoja alipo anatakiwa kupambana na suala hilo kwa kujiajiri kama wanavvyo fanya wanawake hao wa Kata ya Kipawa.
“Kazi ya Serikali ni kuhakikisha inawapunguzia mzigo wananchi kwa kujenga Zahanati, Madarasa, barabara na si kuwanunulia chakula wananchi ambao ni wajibu wao” alisema Dk.Mahanga.
Alisema suala la ajira linachangamoto kubwa si kwa Tanzania bali dunia nzima isipo kuwa linatofautiana kimazingira kwani kwa nchi zilizoendelea wanapo sema hawana ajira ni katika sekta za viwanda, serikali na katika sekta rasmi tofauti na hapa kwetu.
Alisema kwa hapa nchini suala hili ni tete kwa sababu hatuna viwanda vya kutosha na ajira zinazotolewa serikali ni chache hivyo njia pekee ya kujikwamua ni kujiajiri wenyewe kwa kujiingiza katika ujasiriamali.
Dk. Mahanga alitumia fursa hiyo kuwapongeza akina mama hao kwa kuzarisha ajira 300 ambapo kama kila mmoja katika eneo lake la kazi atakuwa na watu wawili anaofanya nao kazi watakuwa na jumla ya watu wenye ajira 600.
Aliwataka wanawake hao kutumia mafunzo hayo kwa kuendelea kufanyakazi kwa bidii na kuwataka vijana kuiga njia hiyo na kujiajiri badala ya kucheza ‘pool’ kutwa nzima huku wakiilalamika serikali kuwa haitoi ajira.
Diwani wa Kata hiyo Bonnah Kaluwa alisema semina hiyo imejumuisha wanawake 300 kutoka katika eneo hilo na kuwa semina nyingine kama hiyo itafanyika mwakani mwezi februari na mafunzo hayo yamedhaminiwa na Benki ya Equity na Darling Hair.
Alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wanawake wajasiriamali wa kata hiyo ili waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali wakati wakifanya biashara zao na kuinua kipato chao na kuwa ukimuinua kiuchumi mwanamke unakuwa umeliinua taifa zima.

No comments:

Post a Comment