Wakina mama wajasiriamali wakiwa katika mafunzo hayo |
Wanawake Wajasiriamali wakisubiri kuingia katika mafunzo hayo |
Na Dotto Mwaibale
NAIBU
Waziri wa Kazi na Ajira Dk.Makongoro Mahanga amesema ukosefu wa ajira hapa
nchini ni jambo tete ambapo kila mtu anatakiwa kujiajiri mwenyewe ili
kukabiliana na sua hilo.
Hayo
aliyasema wakati akifungua mafunzo ya ufundi stadi na ujasiriamali kwa wanawake
wa Kata ya Kipawa Dar es Salaam leo.
Alisema
suala la upatikanaji wa ajiri haipaswi kuachiwa kwa serikali pekee bali kila mtu
mmoja mmoja alipo anatakiwa kupambana na suala hilo kwa kujiajiri kama wanavvyo
fanya wanawake hao wa Kata ya Kipawa.
“Kazi ya
Serikali ni kuhakikisha inawapunguzia mzigo wananchi kwa kujenga Zahanati,
Madarasa, barabara na si kuwanunulia chakula wananchi ambao ni wajibu wao”
alisema Dk.Mahanga.
Alisema
suala la ajira linachangamoto kubwa si kwa Tanzania bali dunia nzima isipo kuwa
linatofautiana kimazingira kwani kwa nchi zilizoendelea wanapo sema hawana
ajira ni katika sekta za viwanda,
serikali na katika sekta rasmi tofauti na hapa kwetu.
Alisema
kwa hapa nchini suala hili ni tete kwa sababu hatuna viwanda vya kutosha na
ajira zinazotolewa serikali ni chache hivyo njia pekee ya kujikwamua ni
kujiajiri wenyewe kwa kujiingiza katika ujasiriamali.
Dk.
Mahanga alitumia fursa hiyo kuwapongeza akina mama hao kwa kuzarisha ajira 300
ambapo kama kila mmoja katika eneo lake la kazi atakuwa na watu wawili anaofanya
nao kazi watakuwa na jumla ya watu wenye ajira 600.
Aliwataka
wanawake hao kutumia mafunzo hayo kwa kuendelea kufanyakazi kwa bidii na
kuwataka vijana kuiga njia hiyo na kujiajiri badala ya kucheza ‘pool’ kutwa
nzima huku wakiilalamika serikali kuwa haitoi ajira.
Diwani wa
Kata hiyo Bonnah Kaluwa alisema semina hiyo imejumuisha wanawake 300 kutoka
katika eneo hilo na kuwa semina nyingine kama hiyo itafanyika mwakani mwezi
februari na mafunzo hayo yamedhaminiwa na Benki ya Equity na Darling
Hair.
Alisema
lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wanawake wajasiriamali wa kata hiyo
ili waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali wakati wakifanya biashara zao na
kuinua kipato chao na kuwa ukimuinua kiuchumi mwanamke unakuwa umeliinua taifa
zima.
No comments:
Post a Comment