Monday, December 24, 2012

MCHORA KATUNI NATHAN MPANGALA, ATEMBELEA WATOTO WANAOENDELEA NA MATIBABU YA SARATANI MUHIMBILI NA KUCHORA NAO


watoto wanaendelea na matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam, wakichora katuni wakati walipotembelewa na mchoraji katuni, Nathan Mpangala kupitia program yake ya Wafanye Watabasamu ambapo pia aliambatana na baadhi ya wachoraji katuni, ndugu na marafiki wa Wafanye Watabasamu, jana.
Mchorajiwa katuni Nathan Mpangala akiangalia jinsi watoto wanavyochora katuni wakati alipowatembelea katika hospitali ya Muhimbili jana
Mtoto Aisha akionesha ufundi wake wa kuchora wakati mchoraji katuni Nathan Mpangala na rafiki zake walipowatembelea na kuchora nao katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jana.
Mtayarishaji na mtangazaji wa kipindi cha Mimi na Tanzania kinachorushwa Chanel 10, Bi. Hoyc Temu, akipata maelekezo ya kitaalam ya jinsi ya kuchora toka kwa mmoja wa watoto wanaoendelea na matibabu ya saratani katika hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam, jana. Matukio ya ziara hiyo yatarushwa na kipindi hiko hivi karibuni.
Mchoraji katuni, Nathan Mpangala kwa kushirikiana wachoraji wenzake, familia, ndugu na marafiki atatembelea watoto wanaosumbuliwa na saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, ikiwa ni muendelezo wa kazi za kijamii kufuatia Tuzo ya Mchoraji Bora wa katuni 2011 aliyopewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) na miaka sita ya Mtukwao maarufu kwa jina la Kibonzo kinachorushwa ITV.
Ziara hiyo ina malengo yafuatayo:
 Kuwapatia wagonjwa zawadi mbalimbali.

  1. Kuchora nao pamoja. Kwa kuwa katuni zina zinachekesha, zitawasaidia watoto hao kupunguza uwoga wa mazingira ya hospitali, zitawasahaulisha maumivu na kuwafanya kuwa bize na kufurahia siku yako.

Katika ziara hiyo Mpangala aliambatana na baadhi ya wachoraji katuni na marafiki wa Programu ya Wafanye Watabasamu na kuwapa zawadi watoto zawadi mbali kisha wakapata nafasi ya kuchora nao michoro ya kawaidha na ile  ihusuyo maisha yao ya kila siku hospitalini hapo.
Kwa niaba ya watoto, Mpangala anaishukuru familia yake, ndugu na marafiki wa Programu ya Wafanye Watabasabu kwa zawadi mbalimbali walizochangia ambazo zimefanya ziara hiyo kuwa ya mafanikio.
Pia anashukuru wachoraji wote waliojitokeza na kuungana naye Muhimbili kwani uwepo wao ulirahisisha usimamiaji wa zoezi la uchorajikwani kila mtoto alisikilizwa pale alipohitaji maelekezo hivyo kufanya watoto.

No comments:

Post a Comment