Monday, December 24, 2012

Umoja wa wapanda pikipiki wa mkoa wa Mwanza kupambana na uhalifu kupitia polisi jamii


Mkurugenzi Msaidizi kutoka  Idara ya Maendeleo ya Vijana  James Kajugusi  (kulia) akimkabidhi mwenyekiti wa Chama cha Umoja wa Waendesha Pikipiki mkoa wa Mwanza Makoye Bunoro Shilingi 50,000/= kwa ajili ya kuweka mafuta katika pikipiki za kitengo cha Polisi jamii pale wanapoenda kupambana na wahalifu.Umoja huo unawasaidia waendesha pikipiki  2034 kupata  leseni na mafunzo yaliyotolewa na Chuo cha VETA kwa gharama naafuu.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka  Idara ya Maendeleo ya Vijana  James Kajugusi  (kulia)  akiongea jambo hivi karibuni na viongozi chama cha Umoja wa wapanda pikipiki wa mkoa wa Mwanza (hawapo pichani) alipowatembelea ofisini kwao eneo la Mlango mmoja ili kuona shughuli zinazofanywa na umoja huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja huo Makoye Bunoro.
Mdhibiti wa mali za chama cha Umoja  wa wapanda Pikipiki wa Mkoa wa Mwanza Faraji Abdalah (kushoto) akimwelezea Mkurugenzi Msaidizi kutoka  Idara ya Maendeleo ya Vijana  James Kajugusi  (kulia)  jinsi umoja huo ulivyoweza kuunda kitengo cha polisi jamii ambacho kinashirikiana na Jeshi la polisi katika kupambana na uhalifu. Katikati ni  Mwenyekiti wa Umoja huo Makoye Bunoro.
Viongozi wa  Umoja wa wapanda Pikipiki wa mkoa wa Mwanza wakimsikiliza  Mkurugenzi Msaidizi kutoka  Idara ya Maendeleo ya Vijana  James Kajugusi  (hayupo pichani)  akiwaeleza jinsi wanavyoweza kuunda SACCOS yao na kukopa fedha kutoka  mfuko wa vijana ambazo zitawasaidia kununua pikipiki zao na kujiajiri wakati alipowatembelea ofisini kwao ili kuona shughuli zinazofanywa na umoja huo.

No comments:

Post a Comment