Saturday, December 8, 2012

NEEMA YAISHUKIA MWANZA TENA, MWAKYEMBE AZINDUA USAFIRI WA TRENI YAKWENDA HUKO.


Waziri wa Uchukuzi,Dk. Harrison Mwakyembe akipeperusha bendera kuashiria uzinduzi wa kuanza tena kwa safari za treni ya abiria kwenda Mwanza.


Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe mwenye suti akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu kabla kuzindua safari ya treni ya abiria kwenda Mwanza leo mchana katika Stesheni ya Dar es Salaam.
 
WAZIRI wa Uchukuzi leo mchana amezindua rasmi usafiri wa treni za abiria toka Dar es Salaam hadi Mwanza, hivyo kutimiza ahadi ya Serikali iliyotolewa Bungeni kipindi cha Bajeti mwaka huu kuhusu
kurejesha huduma hiyo.
Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa amefuatana na viongozi wa Wizara akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara, Injinia Omar Chambo na Mtendaji Mkuu wa TRL, Injinia Kipallo kisamfu aliruhusu treni hiyo kuondoka stesheni ya Dar es Salaam Saa 8:30 mchana huku abiria wakishangilia na kudai huduma hiyo iendelezwe zaidi na zaidi.
Usafiri wa treni ya abiria kati ya Dar na Mwanza ulisitishwa Desemba 2009 kufuatia maamuzi ya iliyokuwa menejimenti ya Kampuni ya  RITES kutoka India .
Treni hiyo ikiwa imefunga Mabehewa 16 yenye abiria wapatao elfu moja inatarajiwa kuingia Mwanza Jumapili asubuhi na kupokewa na Mhe. Naibu Waziri wa UCHUKUZI, Dkt. Charles Tizeba na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mwanza.
Akiongea na viongozi na Wafanyakazi baada ya ufunguzi huo, Dkt. Mwakyembe aliwapongeza Wafanyakazi wa TRL hasa mafundi wa karakana za Dsm na Morogoro kwa kazi kubwa ya kufufua Injini na Mabehewa hivyo kulikolea Taifa mabilioni ya pesa ambazo zingetumika kukodisha vifaa hivyo kutoka Afrika ya Kusini, India ama nchi nyingine.
Treni ya abiria ya Mwanza itakuwepo kwa kuanzia mara mbili kwa wiki Jumanne na Ijumaa kama ilivyo kwa treni ya Kigoma na baadaye kuongezeka jinsi injini na mabehewa yatakavyokuwa yanaongezeka kutengenezwa.

No comments:

Post a Comment