Thursday, January 31, 2013

TAASISI YA THE JOHN MASHAKA YAWAKUTANISHA WAANDISHI NA WATU WENYE ULEMAVU KUJADILI CHANGAMOTO MBALIMBALI

Katibu wa Taasisi ya The john mashaka Bi, Rabia Bakari akiungumza kwa ajili ya kufungua mkutano wa waandishi wa habari na wawakilishi wa vyama vya watu wenye ulemavu ili kujadili kwa pamoja kwa ajili ya ustawi wa wenye ulemavu na wengine wasiojiweza Picha na www.burudan.blogspot.com

Baadhi ya watu wanaotafsili lugha za alama wakiendelea na kazi hiyo wakati wa mkutano

Baadhi ya wawakilishi wakisikiliza kwa makini

Mwenyekiti wa TUSPO Bw. E LLEZER Mdakima kushoto akizungumza wakati wa mkutano huo wengine kulia ni Mjumbe wa Taasisi ya The John Mashaka Bi, Latifa Masasi na Katibu wa taasisi hiyo Bi, Rabia Bakari picha na www.burudan.blogspot.com

"SIKUENDA UINGEREZA KUUZA SURA.." IRENE WOYA





MSANII mahiri wa filamu Irene Uwoya, ameamua kuweka wazi kuwa safari yake aliyowahi kuifanya ya nchini Uingereza mwaka jana kwa ajili ya mazungumzo ya kufanya filamu ya kimataifa bado hayajazaa na matunda na hadi sasa wapo kwenye mazungumzo.

Kauli ya msanii huyo ilimfanya mwandishi wetu amdadisi zaidi, ambapo alisema kuwa kwa sasa kitu wanachokizungumzia ni namna watakavyoandika story ingawa hakutaka kuweka wazi ni story ya namna gani.

Hata hivyo alisema kuwa bado hawajafikia mazungumzo ya kulipwa kiasi gani na lini watafanya lakini anaamini kila kitu kitakuwa safi kwani watu hao wameonesha nia ya kufanya nae kazi.

Pamoja na hayo alishindwa kuwaweka wazi watu hao hata kwa kuwataja majina, kwa madai kuwa kwa sasa siyo wakati wake kwani muda ukifika mashabiki wake watajua anaenda kufanya kazi na kampuni gani.

“Bado tunaendelea na mazungumzo.Sikuenda huko kuuza sura .Najua watu wanasubiri kuona ukweli juu ya maneno yangu haya lakini nachotaka kusema ni kwamba ni kweli nilienda kwa ajili ya mazungumzo ila bado mambo hayajakaa sawa,” alisema Uwoya

DIAMOND ALINASA PENZI LA PENNY WA DTV....NI BAADA YA WEMA, JOKATE,AVRIL NA WENGINE KIBAO




 
Hauwezi kupita mwezi bila kuibuka kitu kitakachomfanya aandikwe tena na tena. 
Katika picha iliyowekwa kwenye ukurasa wa Facebook wa msichana aitwaye Skyner Ally kuna picha inayomuonesha Diamond akiwa amelala usingizi wa pono na msichana anayedaiwa kuwa ni mtangazaji wa DTV, Penny Mungilwa aka Vj Penny.

Picha hii inajieleza yenyewe kwa pozi walilolaa kuwa ni wapenzi ama ni one night stand?
Hata hivyo tulipowasiliana na Penny alisema hiyo ni picha iliyopigwa walipokuwa kwenye scene ya movie wanayoigiza pamoja ambayo amesema hana uhakika lini itatoka!

Penny na Diamond ndani ya movie?????...!!? Ngoja tuisubiri hiyo movie

JACK PATRICK NUSU AMTOE ROHO MTU



 Mrembo aliyenusulika kuuwa na kipigo cha chupa kutoka kwa Jack Patrick, akiwa katika pozi muda mfupi baada ya kushonwa nyuzi tatu.
STAA wa Bongo anayetesa kwenye mitindo, Jacqueline Patrick anakabiliwa na msala wa kumtwanga na chupa nusu kumuua mrembo anayejulikana kwa jina la Hafsa Sasya, Risasi Mchanganyiko linanashuka nayo.
Habari zilizopenyezwa na chanzo chetu kutoka eneo la tukio zinasema kwamba, ishu ilitokea usiku wa kuamkia Jumamosi ya Januari 26, mwaka huu ndani ya Ukumbi  wa Elements Lounge uliopo Masaki, Dar.
CHANZO KINATIRIRIKA
Huku sharti la kutotajwa jina lake gazetini likisisitizwa na chanzo hicho, kilisema: “Unajua yule dada (Hafsa) anasoma Kurasini na anaishi Kijitonyama, namfahamu vizuri sana. Walipokutana na Jack pale ukumbini palitokea kutokuelewana kidogo.

“Baada ya muda hali ikawa sawa, watu wakajua yamekwisa. Jack akaenda zake chooni, aliporudi alikuwa na chupa na kwenda kumpiga nayo Hafsa. Mabaunsa wakamwondoa Jack ukumbini na kumwingiza Hafsa kwenye gari lake kwa lengo la kumpeleka hospitalini. Kilichoendelea hapo sijui.”
PEKUPEKU ZA RISASI
Mwandishi wetu aliingia mzigoni rasmi na kuanza kuichimba kwa kina habari hiyo ambapo alipata uhakika wa kutokea kwa tukio hilo na Jack kufikishwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay ambapo alifunguliwa kesi yenye jalada namba  OB/RB/1678/13  KUJERUHI.
Baada ya kujiridhisha kwa hilo, zoezi lililofuata lilikuwa ni kuwatafuta wawili hao ili waeleze wanachokijua kuhusu tukio hilo. Wa kwanza kupatikana alikuwa ni Jack.
BOFYA HAPA KUMSIKILIZA JACK
“Ni kweli kulitokea ugomvi siku ile...na ni kweli nilihojiwa na Polisi wa Kituo cha Oysterbay, lakini nimetoka kwa dhamana na kesi imekwenda mahakamani.”
HUYU HAPA HAFSA
“Mimi na Jack tulikuwa marafiki lakini nashangaa amenipiga na chupa bila sababu. Nimeshonwa nyuzi tatu. Siku ile alinikuta nimesimama na rafiki yangu mara akanipiga kikumbo kisha akaenda chooni, aliporudi akanikumba tena, nilipomuuliza ikawa kosa; akanipiga na chupa.

“Imeniuma sana maana amenipa jeraha usoni mwangu bila sababu ya msingi, maana sina ugomvi naye. Kwa sababu hili suala lipo mikononi mwa sheria, naamini itachukua mkondo wake.”

Mrembo anayekwenda kwa jina la Hafsa akiwa katika hali mbaya muda mfupi baada ya kushushiwa kipigo kikali na Jack Patrick

MCHUNGAJI AFIKISHWA MAHAKAMANI AKITUHUMIWA KUBAKA NA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI MBEYA




Mchungaji wa Kanisa la EAGT la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi anaetuhumiwa kwa kubaka na kumpa mimba mwanafunzi akitoka mahakamanibaada ya kudhaminiwa
Hapa akiwa anatoka mahakamani baada ya kusomewa mashtaka yake
 Mchungaji wa Kanisa la EAGT la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi (57), Jana alipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya Gilbert Ndeuluwo akituhumiwa  kumbaka na kumpa Mimba mwanafunzi.
Akisoma mashtaka hayo Mwendesha mashtaka wa Serilkali Archiles Mulisa alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo kati ya Mwezi Januari 2008 ambapo alimbaka na kumpa ujauzito Neema Boni (17) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya Sekondari Itende.
Mulisa alidai mahakamani hapo kuwa kosa hilo ni kinyume cha kanuni ya elimu ya 5 ya gazeti la Serikali namba 265 ya mwaka 2003 na chini ya Sheria ya elimu namba 25 ya mwaka 1978 ambapo mshtakiwa anatuhumiwa kutenda makosa mawili ikiwemo kubaka na kusababisha ujauzito.
Aliongeza kuwa kosa la kubaka ni kinyume cha kanuni ya adhabu kifungu cha 130(1),(2)(e) na cha 131(1) kama kilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Hata hivyo mshtakiwa huyo alikana mashtaka yote ambapo  aliachiwa kwa dhamana ya Shilingi Milioni Mbili na mdhamini mmoja mwenye barua kutoka taasisi inayotambulika, kesi hiyo iliahirishwa hadi Januari 30 itakapoanza kusikilizwa.

picha na Mbeya yetu

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii atembelea Hifadhi ya Rabanda



Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Darry Rwegasira katika Hifadhi ya Rabanda-Rumanyika, alipoitembelea kuona shughuli za uhifadhi na kudhibiti ujangili nchini. (Picha zote na Mpiga Picha Wetu)
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akisalimiana na watumishi wa Hifadhi  za Kimisi, Burigi na Biharamulo, Rumanyika alipowatembelea kuona shughuli za uhifadhi na kudhibiti ujangili nchini. 
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiangalia nyaya mbalimbali zilizokamatwa kutoka kwa majangili wanaovamia hifadhi za Burigi na Biharamulo  Rumanyika alipotembelea ili kuona shughuli za uhifadhi na kudhibiti ujangili nchini.

DAR ES SALAAM, Tanzania
SERIKALI imeshangazwa na hatua ya wageni kuwavamia mbuga mbalimbali na misitu nchini kiasi cha kufanya kuongezeka vitendo vya ujangili na kuahidi kuchukua hatua kali ili kutokomeza ujangili huo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema ili kudhibiti hali hiyio hatua za haraka zinahitajika kuchukuliwa ikiwamo na kuimarisha ulinzi katika hifadhi na mapori mbalimbali  ambayo mengine yameanza ktumiwa na waasi.
Akizungumza mjini Bariadi baada ya kuwaona askari wa Kijereshi walioko mahabusu kwa kutuhumiwa kuua majangili, Nyalandu alisema kuwa askari wakliopo ni wachache kiasi cha kufanya majangili wengi kuvamia hifadhi na kuua wanyama hususan tembo.
“Kinachosikitisha ni kuwa hawa majangili wamebadilika zamani waklikuwa wanawinda kwa ajili ya kupata kitoweo lakini sasa wamebadilika na wanavamia kwa silaha za kijeshi na kuua wanyama bila woga” alisema.
Nyalandu aliahidi kuwa kwa sasa hali hiyo imekuwa kama janaga la kitaifa na hivyo kutaka wananchi kubadilika na kkabiliana na majangili ili kulinda maliasili kwa ajili ya vizazi vijavyo.
“Tnahitaji kuajili vijana wengi kadri inavyowezekana ili kukabiliana na wimbi hili, tunahitaji zaidi ya askari 4,000 na kuanzia mwaka huu tumepewa kibakli cha kuajili vijana 400 ambao tutawasambaza katiak hifadhi na mbuga nyingine.
Alisisitiza kuwa kwa sasa askari hao wanalinda zaidi ya kilometa za maraba 169 wakati zinazotakiwa ni kilometa za mraba 25 na hivyo kutoa mwanya kwa majangili kuingina na kutoka bila ya kupatikana.
Nyalandu alisema nchi ilitalajiwa kuwa na tembo 400,000 mwaka huu  miaka 50 iliyopita na kini kutokana na kukithiri vitendo vya ujangili wamebakia tembo 110,000 tu  kitu kinachotishia uwepo wa wanyama hao.

AWAMU YA PILI MRADI WA MAZINGIRA BORA KWA ELIMU BORA.




Mtendaji wa kata ya Kipawa Said Fundi (kulia) akielezea faida faida zilizopatikana kutokana na mradi huo awamu ya kwanza, katikati ni Diwani wa Kata hiyo ambaye ndie mratibu wa mpango huo Bonnah Kaluwa na Meneja wa Matukio wa S&B Marketing Consultancy Regina Ogwal.
Diwani wa kata ya Kipawa Bonnah Kaluwa akifafanua jambo kwenye mkutano huo, kulia ni Mtendaji wa Mtaa Kipawa Said Fundi.
Awamu ya pili ya mradi wa Mazingira Bora kwa Elimu Bora, kwa kata ya Kipawa jijini Dar es Salaam inatarajiwa kuzinduliwa hapo kesho ambapo wadau mbalimbali wakiwemo Watu wa Marekani wamealikwa kushiriki kwenye uzinduzi huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo diwani wa kata ya Kipawa, Bonnah Kaluwa, alisema lengo la mradi huo ni kuboresha Mazingira ya elimu ya Msingi na Sekondari kwenye kata yake.

Aidha Kaluwa alifafanua kuwa Uboreshaji huo wa mazingira ya Elimu unafanyika kwenye Shule saba za Msingi na Sekondary za kata hiyo kwa kuwapatia madawati, maji safi na salama, kujenga vyoo na madarasa pamoja na kuwapatia wanafunzi na walimu vifaa vya elimu.

Awamu ya kwanza ya Mradi huo ilizinduliwa Machi 17,2012 ambapo kwenye awamu hiyo kulifanyika kampeni za kuhamasisha wadau kuchangisha pesa na kufanikiwa kukusanya kiasi cha Tsh.155.5Million, ambazo zilitumika kwa kununua madawati 500 ya Shule ya Msingi, 480 Shule za Sekondari na viti 100 vya shule ya awali pamoja na kufanikiwa kuchimba kisima cha maji katika kila shule.
Awamu hii ya pili ya mradi itajihusisha zaidi kwenye ujenzi wa vyoo na madarasa.

Tuesday, January 29, 2013

MABONDIA WAPIMA UZITO MASHINDANO YA KLABU BINGWA KUANZA KESHO


Bondia Selemani Kidunda wa Klabu ya ngome ambaye aliwakilisha Tanzania katika mashindano ya Olimpic yaliyofanyika London mwaka jana akipima uzito, Dar es salaam Leo kwa ajili ya mashindano ya Klabu bingwa yanayoanza kesho katika uwanja wa ndani wa taifa picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Abdallah Shamte wa Klabu ya Ashanti ya Ilala akipima uzito kwa ajili ya mashindano ya Klabu Bingwa yatakayoanza kesho katika uwanja wa ndani wa Taifa Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

MABONDIA WAPIMA UZITO MASHINDANO YA KLABU BINGWA KUANZA KESHO


Bondia Selemani Kidunda wa Klabu ya ngome ambaye aliwakilisha Tanzania katika mashindano ya Olimpic yaliyofanyika London mwaka jana akipima uzito, Dar es salaam Leo kwa ajili ya mashindano ya Klabu bingwa yanayoanza kesho katika uwanja wa ndani wa taifa picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Abdallah Shamte wa Klabu ya Ashanti ya Ilala akipima uzito kwa ajili ya mashindano ya Klabu Bingwa yatakayoanza kesho katika uwanja wa ndani wa Taifa Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

WAJASIRIAMALI WALIVYONUFAIKA NA SAFARI LAGER WEZESHWA


 Mjasiriamali Elizabeth Chami (26), akioka keki kwenye jiko la kisasa alilozawadiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia promosheni ya Safari Lager Wezeshwa 2012, kwenye karakana yake iliyopo Tabata Mawenzi, Dar es Salaam.
 Mfanyakazi wa karakana hiyo, Happiness akiandaa keki kwenye jiko hilo la kisasa.
 Mfanyakazi wa Kiwanda cha kutangeneza Shampoo  cha L &amp, V Intergrated Firm, kilichopo Mikocheni, Dar es Salaam, Hashim Hussein, akipaki katoni za bidhaa hiyo. Kiwanda hicho kilisaidiwa chupa 15,000 baada ya mmiliki wa kiwanda hicho Valerian Luzangi (hayupo pichani) kuwa mmoja wa washindi wa promosheni  ya Safari Lager Wezeshwa 2012.
 Luzangi, akisaidia kupanga vizuri chupa zilizojazwa shampoo. Kushoto ni mfanyakazi wa kiwanda hicho Stahabu Mwinyi.
 Mjasiriamali Valerian Luzangi (38), kulia, akipanga vizuri katoni za shampoo anazozalisha katika kiwanda chake cha L & V Intergrated Firm, kilichopo Mikocheni, Dar es Salaam juzi. Luzangi alisaidiwa chupa 15,000 baada ya kuwa mmoja wa washindi wa promosheni  ya Safari Lager Wezeshwa 2012, Kushoto ni mfanyakazi wake, Hashim Hussein. 
 Wajasiriamali Innocent Mberwa (kulia) na Gosbert Mugisha, wakiweka sawa mfumo wa umwagiliaji katika moja ya mashamba  ya zao la matikiti maji ya Kampuni yao ya  Tin Wax eneo la Minondo, Kata ya Somangila, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kampuni hiyo ilizawadiwa mfumo huo baada ya kushinda promosheni  ya Safari Lager Wezeshwa 2012. 
 Mjasiriamali Innocent Mberwa akionesha tikiti maji katika moja ya mashamba ya Kampuni yao ya  Tin Wax yaliyopo eneo la Minondo, Kata ya Somangila, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kampuni hiyo ilizawadiwa mfumo wa maji wa umwagiliaji baada ya kushinda promosheni  ya Safari Lager Wezeshwa 2012,
Wajasiriamali Innocent Mberwa (kulia) na Gosbert Mugisha wakiwa sawa mfumo wa umwagiliaji katika moja ya mashamba  zao la matikiti maji ya Kampuni yao ya  Tin Wax eneo la Minondo, Kata ya Somangila, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kampuni hiyo ilizawadiwa mfumo huo baada ya kushinda promosheni  ya Safari Lager Wezeshwa 2012,
Baadhi ya vitunguu vinavyozalishwa katika shamba hilo. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO.

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MKUTANO WA KANDA WA MASHAURIANO WA BARAZA LA VIJANA WA JUMUIYA YA MADOLA .


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua Mkutano  wa  Mashauriano wa Kanda wa  Baraza la Vijana wa Jumuiya ya Madola uliofunguliwa leo Januari 29, 2013 katika Hoteli ya White Sands  jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara, akizungumza wakati wa Mkutano  wa  Mashauriano wa Kanda wa  Baraza la Vijana wa Jumuiya ya Madola uliofunguliwa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katika Hoteli ya White Sands  jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel, wakati wa ufunguzi wa Mkutano  wa  Mashauriano wa Kanda wa  Baraza la Vijana wa Jumuiya ya Madola uliofunguliwa leo, katika Hoteli ya White Sands  jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Dkt. Mohammed Gharib Bila, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo leo, katika Hoteli ya White Sands  jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Dkt. Mohammed Gharib Bila, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo leo, katika Hoteli ya White Sands  jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Dkt. Mohammed Gharib Bila, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo leo, katika Hoteli ya White Sands  jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo, wanaowakilisha makundi mbalimbali ya vijana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo, wanaowakilisha makundi mbalimbali ya vijana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo, wanaowakilisha makundi mbalimbali ya vijana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mkurugenzi wa Maendelea ya Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel, baada ya kufungua mkutano wa  Mashauriano wa Kanda wa  Baraza la Vijana wa Jumuiya ya Madola uliofunguliwa leo, katika Hoteli ya White Sands  jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara.

LULU ACHEKA DAKIKA MOJA.... KISHA AMKUMBATIA MAMA YAIKE NA KUMWAGA MACHOZI MFULULIZO KWA FURAHA HUKU ASIAMINI KUWA KWELI KAACHIWA KWA DHAMANA KAT8IKA KESI INAYOMUANDAMA YA KUMUUA KANUMBA BILA KUKUSUDIA... AONDOKA KORTINI MGARI WA KISASA AINA TOYOTA LAND CRUISER




Lulu akitoa neno la shukrani kupitia vyombo vya habari baada ya kutolewa jela kwa dhamana leo



Mama lulu akifurai baada ya kukutana tena na mwanae ambapo walitenganishwa takribani miezi nane na mtoto wake












Mama lulu kushoto lulu mwenyewe katikati na Muhsin Awadhi Dkt Cheni ambaye ni mtu wa karibu wa familia hiyo ya lulu wakitoka mahakama kuu leo



Lulu alionekana akicheka kwa furaha ya kuachiwa huru kwa dhamana kwa dakika chache leo alasiri akiwa na mama yake Lucrecia Kalugila, lakini muda mrefu baadaye wakajikuta wakibubujikwa na machozi bila breki ikiwa ni matokeo ya kuzidiwa na hisia za furaha hiyo huku pia wakionekana kutoamini juu ya kile kilichotokea.

Msanii huyo nyota wa filamu nchini, ameachiwa kwa dhamana hatimaye baada ya kutimiza masharti aliyiopewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam katika kesi inayomkabili ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake nyota, marehemu Steven Kanumba.

Awali, mama huyo wa Lulu, ndugu, jamaa, marafiki na wasanii mbalimbali wa filamu nchini walionekana mahakamani tangu saa 2:30 asubuhi jana, lengo likiwa ni kujua hatma ya mpendwa wao ambaye amekuwa akisota mahabusu tangu Aprili mwaka jana.

Baadaye, mama huyo alionekana kujawa na hisia kali kiasi cha kumwaga machozi yatokanayo na furaha aliyokuwa nayo baada ya mahakama kumuachia binti yake kwa dhamana na wote wawili kuonekana wakikumbatiana; kama watu wasioamini juu ya kile kilichotokea.

ILIVYOKUWA
Lulu mwenye miaka 18, anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya bila kukusudia ya msanii mwenzake, Kanumba (28), aliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti aliyopewa.

Msanii huyo alifikishwa saa 7:50 mchana akitokea mahabusu ya gereza la Segerea, akiwa katika ‘deffender’ jeupe la Magereza lenye namba za usajili STK 2823.

Mawakili wa pande zote walihakiki nyaraka za dhamana. Ilipofika saa 9:10 alasiri, Lulu alipandishwa kizimbani akiwa na wadhamini wake.

Mbele ya Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Francis Kabwe, Lulu aliwawakilisha na wadhamini wawili, James Mboneka kutoka Wizara ya Afya na Florian Mutafungwa wa Wizara ya Ardhi.

Saa 9:20, Lulu alikamilisha taratibu za mahakama na kuachiwa huru hatimaye ambapo mama yake (Lucrecia), ndugu, jamaa na marafiki zake walijikuta wakiangua kilio cha furaha.

Akizungumza baada ya kuwa huru kwa dhamana, Lulu alisema anamshukuru Mungu pamoja na watu wote walio pamoja naye katika kipindi chote kigumu.
"Sina la kusema... nawashukuru wote waliokuwa pamoja na mimi tangu nilipopata kesi hii. Ila bado nawaomba waendelee kuniombea kwa sababu nimepata dhamana tu, bado nina safari ndefu. Kesi  bado mbichi, niombeeni jamani," alisema Lulu huku akilia kabla ya kuondoka kwenye viunga vya mahakama hiyo akiwa ndani ya
gari lenye namba za usajili T 480 CFX, Toyota Land Cruser (V8) la rangi ya kijivu.

Wakili wa utetezi, Peter Kibatala alisema dhamana ni mchakato wa kisheria unaotakiwa kufuatwa katika mahakama na kwamba mteja wao amefanikiwa kupata dhamana na sasa wanasubiri wito wa mahakama wakati itakapopanga tarehe kwa ajili ya kusikiliza ushahidi wa Jamhuri wa kesi ya msingi.
Mapema Juzi, Jaji Zainabu Mruke alitoa masharti ya dhamana kwa mshtakiwa huyo baada ya wakili wa utetezi Peter Kibatala kuwasilisha maombi ya dhamana kwa hati ya dharula chini ya kifungu cha 148 kidogo cha (1) na cha (2) cha Mwenendo wa Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA).

Jaji Mruke alisema kosa linalomkabili  mshakiwa lina dhamana kisheria na kwamba mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa kufuata masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali watakaosaini  hati ya dhamana ya Sh. milioni 20 kila mmoja.

Alitakiwa pia awasilishe hati zake za kusafiria, kuripoti kila tarehe Mosi ya mwezi kwa Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na asitoke nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila kibali cha msajili huyo.
Katika kesi ya msingi, Lulu anadaiwa kuwa  Aprili 7, 2012, katika eneo la Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam, alimuua Kanumba bila kukusudia.