Wednesday, January 30, 2013

MCHUNGAJI AFIKISHWA MAHAKAMANI AKITUHUMIWA KUBAKA NA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI MBEYA




Mchungaji wa Kanisa la EAGT la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi anaetuhumiwa kwa kubaka na kumpa mimba mwanafunzi akitoka mahakamanibaada ya kudhaminiwa
Hapa akiwa anatoka mahakamani baada ya kusomewa mashtaka yake
 Mchungaji wa Kanisa la EAGT la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi (57), Jana alipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya Gilbert Ndeuluwo akituhumiwa  kumbaka na kumpa Mimba mwanafunzi.
Akisoma mashtaka hayo Mwendesha mashtaka wa Serilkali Archiles Mulisa alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo kati ya Mwezi Januari 2008 ambapo alimbaka na kumpa ujauzito Neema Boni (17) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya Sekondari Itende.
Mulisa alidai mahakamani hapo kuwa kosa hilo ni kinyume cha kanuni ya elimu ya 5 ya gazeti la Serikali namba 265 ya mwaka 2003 na chini ya Sheria ya elimu namba 25 ya mwaka 1978 ambapo mshtakiwa anatuhumiwa kutenda makosa mawili ikiwemo kubaka na kusababisha ujauzito.
Aliongeza kuwa kosa la kubaka ni kinyume cha kanuni ya adhabu kifungu cha 130(1),(2)(e) na cha 131(1) kama kilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Hata hivyo mshtakiwa huyo alikana mashtaka yote ambapo  aliachiwa kwa dhamana ya Shilingi Milioni Mbili na mdhamini mmoja mwenye barua kutoka taasisi inayotambulika, kesi hiyo iliahirishwa hadi Januari 30 itakapoanza kusikilizwa.

picha na Mbeya yetu

No comments:

Post a Comment