Wednesday, January 30, 2013

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii atembelea Hifadhi ya Rabanda



Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Darry Rwegasira katika Hifadhi ya Rabanda-Rumanyika, alipoitembelea kuona shughuli za uhifadhi na kudhibiti ujangili nchini. (Picha zote na Mpiga Picha Wetu)
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akisalimiana na watumishi wa Hifadhi  za Kimisi, Burigi na Biharamulo, Rumanyika alipowatembelea kuona shughuli za uhifadhi na kudhibiti ujangili nchini. 
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiangalia nyaya mbalimbali zilizokamatwa kutoka kwa majangili wanaovamia hifadhi za Burigi na Biharamulo  Rumanyika alipotembelea ili kuona shughuli za uhifadhi na kudhibiti ujangili nchini.

DAR ES SALAAM, Tanzania
SERIKALI imeshangazwa na hatua ya wageni kuwavamia mbuga mbalimbali na misitu nchini kiasi cha kufanya kuongezeka vitendo vya ujangili na kuahidi kuchukua hatua kali ili kutokomeza ujangili huo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema ili kudhibiti hali hiyio hatua za haraka zinahitajika kuchukuliwa ikiwamo na kuimarisha ulinzi katika hifadhi na mapori mbalimbali  ambayo mengine yameanza ktumiwa na waasi.
Akizungumza mjini Bariadi baada ya kuwaona askari wa Kijereshi walioko mahabusu kwa kutuhumiwa kuua majangili, Nyalandu alisema kuwa askari wakliopo ni wachache kiasi cha kufanya majangili wengi kuvamia hifadhi na kuua wanyama hususan tembo.
“Kinachosikitisha ni kuwa hawa majangili wamebadilika zamani waklikuwa wanawinda kwa ajili ya kupata kitoweo lakini sasa wamebadilika na wanavamia kwa silaha za kijeshi na kuua wanyama bila woga” alisema.
Nyalandu aliahidi kuwa kwa sasa hali hiyo imekuwa kama janaga la kitaifa na hivyo kutaka wananchi kubadilika na kkabiliana na majangili ili kulinda maliasili kwa ajili ya vizazi vijavyo.
“Tnahitaji kuajili vijana wengi kadri inavyowezekana ili kukabiliana na wimbi hili, tunahitaji zaidi ya askari 4,000 na kuanzia mwaka huu tumepewa kibakli cha kuajili vijana 400 ambao tutawasambaza katiak hifadhi na mbuga nyingine.
Alisisitiza kuwa kwa sasa askari hao wanalinda zaidi ya kilometa za maraba 169 wakati zinazotakiwa ni kilometa za mraba 25 na hivyo kutoa mwanya kwa majangili kuingina na kutoka bila ya kupatikana.
Nyalandu alisema nchi ilitalajiwa kuwa na tembo 400,000 mwaka huu  miaka 50 iliyopita na kini kutokana na kukithiri vitendo vya ujangili wamebakia tembo 110,000 tu  kitu kinachotishia uwepo wa wanyama hao.

No comments:

Post a Comment