Thursday, January 24, 2013

MAANDALIZI YA MAULID YA MTUME MOHAMAD (S.A.W) VIWANJA VYA MNAZIMMOJA LEO


Eneo la viwanja vya Mnazimmoja jijini Dar es Salaam likiandaliwa kwa mapambo kwaajili ya maandalizi ya Maulid ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) hapo kesho ambapo waisilamu duniani kila inapofika mwezi wa mfungo sita hukusanyika kwenye maeneo mbalimbali kusoma maulid ya kukumbuka kuzaliwa kwa Mtume wao. Sherehe hizo kitaifa mwaka huu zinatarajiwa kufanyika Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.
Baadhi ya maeneo yalikuwa tayari kwenye viwanja  hivyo yanavyoonekana mchana waleo huku maeneo mengine yakiendelea kupambwa tayari kusubiri siku ya kesho ambayo ni mapumziko ya kitaifa kutokana na Maulid hayo.
Vijana waliopewa dhamana ya kupamba eneo la viwanja vya Mnazi Mmoja wakiendelea na kazi hiyo leo, ambapo wanaendelea na ufungaji wa taa ili huduma ya umeme iwepo ya kutosha.
Vijana waliopewa kazi ya kukata nyasi ndani ya viwanja hivyo wakiendelea na kazi ili kuwe na eneo la kutosha kutoka na wakazi wa jiji la Dar hufurika kwenye viwanja hivyo.
Mitaa ya Kariakoo ikiwa kwenye mwonekano wa mapambo kwa zaidi ya wikimbili sasa kutokana na kuukaribisha mwezi wa mfungo sita ambao hufanyika maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhamad (SWA), Watu mbalimbali wamekua wakizishangaa bendera zinazopamba eneo la Kariakoo na hapa ni kwenye makutano ya barabara ya Bibi titi na Uhuru.
Maeneo mengine kwenye viwanja hivyo yamewekwa maturubai kwaajili ya kuzuia mvua kama itanyesha

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limetangaza Maulid ya Mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W) yatasomwa usiku wa Januari 24.

Taarifa katika vyombo vya habari iliyotolewa jana na kusainiwa na Katibu Mkuu wa Bakwata, Suleiman Lolila, ilieleza maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika wilayani Mkuranga, Pwani.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa, baada ya kusomwa kwa Maulid hayo, yatafuatiwa na Baraza la Maulid litakalofanyika Januari 25, majira ya sasa 9 alasiri.

Taarifa hiyo ilieleza katika maadhimisho hayo, Waislamu watajifunza mengi juu mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W) na kuyafuata kama ilivyoagizwa katika vitabu vyake vitukufu.

“Bakwata linawataka waumini kuadhimisha siku hiyo na kupata mawaidha mbalimbali ambayo yatatolewa. Tunawatakia maandalizi mema ya sikukuu hiyo,” ilieleza taarifa hiyo ya Bakwata.

No comments:

Post a Comment