Tuesday, January 8, 2013

WANNE WASHIKILIWA KWA KUTELEKEZA ABIRIA NA KWENDA KUBEBA GONGO!


Na Abdulaziz,Lindi
WATU wanne pichani wakiwemo watumishi wa basi dogo aina ya Hiace,wakazi wa mkoa wa Mtwara, wanashikiliwa na Polisi mkoani Lindi, kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za kuwatelekeza abiria njiani kwa ajili ya kwenda kupakia na kubeba pombe haramu ya moshi (gongo).
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoani hapa,George Mwakajinga,zinaeleza watuhumiwa hao wote wakazi wa mkoa wa Mtwara, Mwakajinga amewataja wanaowashikilia kuwa ni pamoja na dereva na
kondakta wa Hiace, Shaibu Daudi (30),John Mbena Saidi (25),Mariamu Yassini Mautila (36) wakazi wa Ligula,na Habiba Maulidi Sijaona (28) wafanyabiashara ya Pombe ya moshi (Gongo) mkazi wa mtaa wa
majengo,Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kulitokana na kitendo kilichofanywa na wafanyakazi wa gari hiyo kuwashusha na kuwatelekeza njiani abiria waliokuwa wamewabeba kuelekea mkoani Mtwara,na kwenda kijiji cha Ruhokwe kilichopo wilaya ya Lindi,kubeba pombe haramu ya
moshi (gongo).
Mwakajinga akasema Hiace hiyo,ambayo mlango mkubwa wa nyuma umeandikwa neno lisemalo,Simba wa Yuda,yenye namba za usajili T 436BJV,inamilikiwa na mfanyabiashara aitwae D.D. Chigumila wa mjini
Mtwara,ilikuwa imebeba zaidi ya abiria 20, wakitoka mjini Lindi kwenda mkoani Mtwara.

No comments:

Post a Comment